Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la
Livingstone Mshiri (56) Mkazi wa Sumbawanga Rukwa
amekutwa akiwa amefariki Dunia
katika Nyumba ya kulala wageni
akiwa na mpenzi wake
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari tukio
hilo lilitokea hapo
Novemba saba majira ya saa 11 alfajiri katika nyumba ya kulala wageni inayoitwa Manungu iliyoko katika
Mtaa wa Majengo B Kata ya
Kashaulili mjini Mpanda
Alisema
marehemu alikutwa akiwa amefariki
Dunia huku akiwa
katika chumba namba
nne katika nyumba
hiyo ya kulala wageni akiwa
chumbani na mpenzi wake
aitwaye Jovina Mathias (19)
Mkazi wa Kijiji
cha Mtisi Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi
Alifafanua
kuwa marehemu na
mpenzi wake huyo walikuwa
wamefikia kwenye nyumba
hiyo ya kulala wageni
kwa muda wa siku mbili
Kidavashari alieleza kuwa chanzo
cha tukio la kifo
hicho bado hakijajulikana na
polisi wanaendelea na
uchunguzi ili kuweza
kubaini chanzo kilichopelekea kifo cha Marehemu
Na
jeshi la Polisi
Mkoa wa Katavi
linamshikilia mtuhumiwa Jovina
Mathias ambae alikuwa mpenzi wa marehemu kwa mahojiano zaidi kuhusiana na kifo hicho
No comments:
Post a Comment