Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Msimamizi wa uchaguzi wa Majimbo ya Katavi na
Kavuu Mkoani hapa ambae pia ni
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mlele Razalo Bene amewakaidhi hati za ushindi wabunge wateule na Madiwani wa
Majimbo hayo
Msimamizi huyo wa
uchaguzi aliwakaidhi hati
hizo hapo jana
kwa nyakati tofauti kwenye majimbo majimbo ya Kavuu katika Tarafa ya Mpimbwe na Katavi
katika ofisi za Halmashauri ya
Wilaya ya Mlele huko Inyonga
Kwa upande wa
jimbo la Katavi msimamizi
huyo alikadhi hati ya
ushindi kwa Mbunge mteule wa
Jimbo hilo Mwandisi Izack
Kamwelwe(CCM) na Madiwani wa
Kata sita za Jimbo
hilo
Jimbo la
Kavuu alikabidhi hati ya
ushindi kwa Mbunge
mteule wa jimbo la Kavuu Dr Pudensiana Kikwembe (CCM) pamoja
na madiwani tisa wa jimbo hilo
Akizungumza mara
baada ya kukabidhiwa hati
ya ushindi Mbunge mteule wa Jimbo la
Katavi Mwandisi Kamwelwe
alisema uchaguzi katika
jimbo la Katavi
ulikuwa huru na haki
Alisema
kwenye jimbo hilo
taratibu zilifuatwa na
ndio maana wagombea
wa jimbo hilo hawakuweza kugombana
katika mchakato wote
wa uchaguzi kwenye jimbo
hilo
Kazi
iliyopo mbele yao viongozi
waliochaguliwa ni kuwatumikia wananchi wote
bila kujali itikadi
za vyama vya
alisema Mwandisi Kamwelwe
Jumla ya
vyama vitatu vya
siasa vya CCM, CHADEMA
na ACT Wazalendo vilishiriki
uchaguzi huo ambapo
Chama cha Mapinduzi kilishinda
ubunge kwenye majimbo hayo
na nafasi za
udiwani kwenye Kata
zote za wameshinda
wagombea wa CCM
No comments:
Post a Comment