Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
ALIGOMBEA UBUNGE(ACT WAZALENDO) KUANZA KEMPENI WIKI
IJALO KWA AJIRI YA UCHAGUZI MKUU WA 2020
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Aliyekuwa mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kavuu la Kavuu Mkoa wa Katavi katika uchaguzi mkuu wa Oktoa 25 mwaka huu
kupitia Chama cha ACT WAZALENDO Stansilaus Kisesa amehaidi kuanza kempeni
wiki ijalo kwa ajiri ya maandalizi ya kugombea Ubunge wa Jimbo hilo katika uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2020
Kisesa
alitowa kauli hiyo ya kuanza kampeni
wiki ijalo wakati alipokuwa akizungumza hapo
jana na Waandishi wa Habari hapo jana kwenye hotel ya
Victoria Mjini hapa
Alisema kuwa
anatarajia kuanza kuanza kampeni
za kugombea ubunge wa Jimbo la Kavuu ikiwa ni maandalizi ya kugombea tena
kwa mara ya pili jimbo
hilo katika uchaguzi mkuu ujao
wa mwaka 2020
Alifafanua kuwa katika
uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka huu hakuweza kufanya vizuri
na ndio maana
ameamua kuanza kampeni
za kugombea jimbo hilo mapema
Alisema
lengo lake la
kugombea ubunge kwenye
jimbo hilo katika uchaguzi mkuu uliopita
ilikuwa ni kutangaza kwanza jina
lake na Chama chake
cha ACT WAZALENDO kwa ajiri
ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa
mwaka 2020
Kama jina langu
na chama changu
tayari tumetangazika sioni sababu ya kutoanza kampeni wiki
ijalo ili nijiandae na
uchaguzi ujao alisema Kisesa
Katika uchaguzi
wa kugombea ubunge wa
jimbo hilo mgombea ubunge (CCM)
Pudensiana Kikwembe alishinda
kwa kupata kura 18,009 akifuatiwa na
mgombea wa CHADEMA
Laulenti Mangweshi aliyepata kura 11,185 na
Stansilaus Kisesa ACT WAZALENDO alipata kura 202
Jimbo hilo
la Kavuu katika
uchaguzi wa Oktoba 25 lilikuwa na
wagomea wa nafasi ya ubunge watatu kutoka vyama
vya CCM, CHADEMA na ACT
Wazalendo
No comments:
Post a Comment