Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Muluchuma
Katavi
Waliokuwa Raia wa Nchi ya Burundi ambao hivi karibuni wamepewa uraia wa Tanzania
wanaoishi kwenye
Makazi ya Wakimbizi ya Mishamo Wilayani
Mpanda wameiomba Serikali kuharakisha mchakato wa
kubadili hadhi ya Makazi
hayo kutoka makazi ya wakimbizi kuwa
maeneo maeneo yanayoendeshwa
chini ya Serikali za Mitaa kama yalivyo maeneo mengine ya Tanzania
Ombi la Raia wapya wa Tanzania lilitolewa hapo jana kwenye risala yao iliyosomwa na
Agustino Thabiti mbele ya
Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa sherehe zilizoandaliwa na Raia hao wapya waliokuwa wakiishukuru Serikali ya Tanzani
kwa kuwapatia Urai watu Tanzania watu
wapatao 52,594 zilizofanyika katika uwanja wa Mishamo
Walieleza lengo la kubadili makazi hayo ni kurahisisha upatikanaji
wa hudumu za jamii na utenganisho
wao na jamii inao wazunguka
Kufuatia
kutangazwa kwa maeneo mapya ya kiutawala
katika ngazi ya Tarafa ,Kata
na Vjiji mwezi june 2015
wanaishukuru Serikali kwani kutokana na
tangazo hilo tayari wameshiriki kwa mara
ya kwanza kupiga kura ya kuwachagua
Viongozi katika uchaguzi wa Mkuu wa
oktoba 25 mwaka huu
Na katika
uchaguzi huo wamepata Madiwani wanne katika Kata nne zilizopo kwenye Makazi hayo ya Wakimbizi ya Mishamo yalionzishwa mwaka 1978
hivyo wanaishukuru Serikali ya Tanzania
kwa kuendelea kuongeza
maeneo mapya ya kiutawala
Pia waliiomba Serikali kuona umuhimu wa kuwasogezea huduma
za Kibenki kwani mahitaji yao ni makubwa kwa ajiri ya usalama wao na fedha zao
hivyo wanalazimika kufuata huduma
za kibenki mjini Mpanda umbali wa kilometa 145
na Mkoa wa jirani wa Kigoma
Kwa upande wake
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema Serikali ya Tanzania namna
ya kuwafanya watu hao walipewa
vyeti vya uraia wa Tanzania ili waweze
kuishi vizuri kama raia wengine
Alisema
wapo watu 3700 ambao ni Raia wa Nchi ya Burundi wanaoishi
kwenye makazi hayo waliomba kupatiwa
uraia wa Tanzania lakini
wameshindwa kupatiwa uraia kutokana na
taratibu zao kutokamilika hivyo ni
vizuri wakamilishe taratibu
ili nao waweze kupatiwa uraia kama wenzao
Alifafanua
wapo watu 75 waliomba kurudi
Nchini kwao Burundi lakini mpaka sasa watu hao bado wanaendeleea kuishi
kwenye makazi hayo na baadhi yao wamegunduliwa kuwa sio Raia wa Burundi mbali ni Raia wa Nchi ya Kongo hivyo kama
wameamua kuishi hapa nchini wafuate taratibu
vinginevyo Serikali itawachukulia hatua
No comments:
Post a Comment