Home » » MATOKEO YA UCHAGUZI MAJIMBO YA KATAVI

MATOKEO YA UCHAGUZI MAJIMBO YA KATAVI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Walter  Mguluchuma
Katavi yetu blog
Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Mpanda Mjini amemtangaza Sebastiani Kapufi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini jimbo ambalo limeongozwa kwa kipindi cha miaka 10 na  Said Arfi  CHADEMA
Kapufi(CCM) amepata kura 29,193  Jonas Kalinde  kura 18,649,  (   CHADEMA)Galus Mgawe 1449 (ACT) na  Mussa Kasogela kura  228(ADC)
Mkurugenzi wa uchaguzi wa Majimbo ya Katavi na Kavuu Lazalo Bene ametangaza matokeo  ya ubunge katika majimbo hayo   la  Katavi Aizack  Kamwele (CCM) Kura  8,956 George  Shambwe( CHADEMA) kura 3,491 na Lucas  Pinda (ACT) kura  566
 Jimbo jipya la Kavuu matokeo yake  ni kama yafuatayo Pudensiana Kikwembe (CCM) kura18,009 Laulent  Mangweshi (CHADEMA)kura 11,185 na Sitansilaus Kisesa (ACT) kura  205
Msimamizi wa Jimbo la Mpanda Vijijini Astom Chang’a ametangaza  matokeo ya ubunge kama ufuatavyo  Moshi Kakoso     ( CCM  kura  30,512   Mussa   Masanja  CHADEMA kura  16,454 na  Anastela Malack  ACT  kura 2854
Msimamizi wa Jimbo la Nsimbo ametangaza matokeo  ya jimbo hilo ambapo Richald Mbogo  CCM amepata kura 30,292  Gelard  Kitabu  CHADEMA  kura   6,879 na  Elias  Kifunda  ACT
 amepata kura  399
Mkoa wa Katavi unajumla ya majimbo matano ambayo yote yamechukuliwa na wagombea Ubunge wa CCM

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa