Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mahakama ya Wilaya
ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemuhukumu
Maiko Bundala (26) Mkazi wa Kijiji
cha Mnyagala Wilaya ya Mpanda kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana
na hatia ya kumbaka mtoto (8) na
kumuharibu vibaya katika sehemu zake za
siri
Hukumu hiyo
iliyovutia hisia za watu wengi wa Mji wa Mpanda ilitolewa hapo jana na Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya kulidhika na ushahidi uliotolewa
Mahakamani hapo wa upande wa mashitaka na utetezi
Awali katika kesi hiyo Mwanasheria wa Serikali
Kulwa Kusekwa alidai
mahakamani hapo kuwamshitakiwa alitenda kosa hilo hapo Machi
27 mwaka huu majira ya saa kumi na mbili jioni
Siku hiyo mtoto
huyo aliyebakwa alikuwa akicheza katika
eneo la nyumba ya mshitakiwa huku
akiwa na watoto wenzake wa eneo hilo
Alidai kuwa
ndipo Bundala alipowatuma watoto
waliokuwa wakicheza na mtoto aliyembaka wakanunue pipi dukani na yeye alibaki na
mtoto huyo
Alieleza
kuwa baada ya kuona amebaki na mtoto huyo alimwingiza
ndani ya chumba chake na kisha
alimvua nguo kwa nguvu huku na kisha
alianza kumbaka huku akiwa amemziba mdomo
iliasipige kelele
Katika ushahidi alioutowa Mahakamani hapo mama wa mtoto
aitwaye Sofia Masanja aliiambia Mahakama kuwa siku hiyo ya
tukio mtoto wake alikuwa akicheza katika
eneo la nyumba ya mtuhumiwa huku akiwa
na watoto wenzake
Alidai kuwa baada ya kuona mtoto wake amechelewa aliamua
kumfuata alikuwa akicheza na wenzake
na alipofika kwenye nyumba ya
Bundala alikuta wale watotowote hawapo na alisikia mtoto akilia hivyo hakujua
kama ni mtoti wake
Alieleza kuwa baada ya muda mfupi mtoto
wake alirudi nyumbani huku analia
na alimweleza Mama yake kuwa Bundala amemuingizia sehemu zake za siri na
amemuumiza kwenye sehemu zake za siri
hari ambayo ilimfanya mama wa mtoto huyo
kuanza kulia huku akielekea kwa
mtendaji wa Kijiji
Baada ya kufikishwa kwenye uongozi wa Kijji mshitakiwa alikana kumbaka mtoto huyo na ndipo walipoamua mshitakiwa afikishwe katika kituo cha Polisi cha Wilaya ya Mpanda
Shahidi wa tano wa kesi hiyo ambae ni daktari alidhibitisha Mahakamani hapo kuwa vipimo alivyofanyiwa mtoto huyo vilionyesha kuwa mtoto huyo alikuwa
ameingiliwa katika sehemu zake za siri na kuharibiwa
Katika
utetezi wake Mahakamani hapo mshitakiwa
aliomba Mahakama imwachie
huru kwani yeye hakutenda kitendo hicho
isipo kuwa alikuwa anakuwa
akimdai fedha mama wa mtoto huyo ndio maana
aliamua kumsingizia kuwa amembaka
mtoto wake
Baada ya
utetezi huo ambao ulipingwa vikali
na Mwanasheria wa Serikali Kulwa Kesekwa
na aliiomba Mahakama itowe itowe
adhabu kali kwa mshitakiwa kwani tabia
ya kuwabaka watoto wadogo inaonekana
kushamiri katika Wilaya ya Mpanda
Hakimu Chiganga baada ya kuzisikiliza pande zote mbili za utetezi na mashitaka aliiambia Mahakama kuwa Mahakama bila shaka yoyote imetia hatiani mshitakiwa kwa kosa
la kuvunja sheria no 130(1) (2)k na 131(1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2002
Hivyo kutokana
na kosa hilo Mahakama imemuhukumu
Maiko Bundala kutumikia jela kifungo cha maisha jela kuanzia jana
0 comments:
Post a Comment