Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Wakazi wa Mkoa wa
Katavi wametakiwa kutii maelekezo
yanayotolewa na Tume ya Taifa ya uchaguzi
ili wasivilazimishe vyombo vya
ulinzi na usalama vitumie nguvu pasipo
kuwa na sababu
Wito huo
umetolewa hapo jana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Mwandisi Emanuel
Kalobelo wakati wa kikao cha wadau wa
amani kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda
Alisema endapo wananchi wa Mkoa wa Katavi
watatii maelekezo yanayotolewa na Tume
ya Taifa ya uchaguzi kwa ajiri ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 kutakuwa na
uwezekano wa kufanya kwa uchaguzi wenye
amani
Mwandisi Kalobelo
aliwaeleza wajumbe wakikao hicho kuwa
endapo wananchi haatatii maelekezo
yanayotolewa na tume ya Taifa ya uchaguzi kutakuwa na kila dalili za uvunjikaji
wa amani na matokeo yake wananchi
watakuwa wamevilazimisha vyombo vya
ulinzi na usalama kutumia nguvu
pasipo sababu yoyote
Nae Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri
Kidavashari alieleza kuwa Tume ya uchaguzi imeisha towa maelekezo ya kuwataka
wananchi wasikae karibu na vituo vya kupigia kura na badala yake wakipiga kura warudi makwao au
kwenye biashara zao licha ya kanuni ya uchaguzi kuruhusu watu wakae umbali wa
mita 200 kutoka eneo la kituo cha kupigia kura
Alisema kuwa
sheria Namba 73 inawapa mamlaka jeshi la
Polisi kuzuia mikusanyiko ya makundi ya watu
ambao wanaweza kusababisha
uvunjikaji wa amani
Kwaupande wake
Vicenti Nkana alisema kuwa kila mzazi
Mkoani Katavi anao wajibu wa
kuwaonya watoto kutofanya siku ya uchaguzi wa Oktoba 25 yale
ambayo yamekazwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi
Alisema
kama viongozi wa vyama vya siasa watajitambua kuwa wapo kwa ajiri ya manufaa ya Taifa wakijitambua hivyo uchaguzi mkuu utakuwa wa
amani na utulivu
Katika kikao
hichoviongozi wa vyama vya upinzani
walikuwa wakitetea kuwa watu
waruhusiwe kukaa umbali wa mita 200
kutoka kwenye vituo vya kupigia kura kama ambavyo kanuni yatume ya uchaguzi inavyoeleza hata hivyo wajumbe wengi wa kikao hicho
walipinga hoja hiyo kwa kile walichodai
kuwa wakiruhusiwa kukaa umbali huo upo uwezekano wa kutokea kwa uvunjikaji wa
amani
Kikao hicho chenye lengo la kujadili hari ya usalama na
amani wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi kiliwashirikisha wajumbe wa
kamati za ulinzi na usalama wa Wilaya zote za Mkoa wa Katavi ,wajumbe wa
kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa Katavi
viongozi wa tume ya Taifa ya uchaguzi, viongozi wa madhehebu ya Dini
wazee maarufu na Waandishi wa Habari
0 comments:
Post a Comment