Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
N a Walter
Mguluchuma
Katavi
Jumla ya
watu 3,870 walioandikishwa kupiga kura kwa ajiri ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25
wamebainika wakiwa sio Raia wa
Tanzania na vitambulisho vyao
vimerejeshwa kwa Tume na wameondolewa kwenye
Daftari la wapiga kura
Hayo yalisemwa
hapo jana na
Afisa wa wa tume ya uchaguzi wa
Kanda ya
nyanda za juu Jane Tungu
kwenye hutuba yake ya ufunguzi
wa mkutano wa tume
na viongozi wa vyama vya siasa
wa Mkoa wa Katavi uliofanyika
katika ukumbi wa Chuo Kikuu huria
cha Mkoa wa Katavi
Alisema baada ya
kuchakata Daftari mchakato wa mwisho wa kuhakiki Daftari hatimae
idadi halisi ya wapiga kura
katika daftari la kudumu la wapiga kura idadi yao ni
watu 23,154,485 ambapo waliojiandikishwa na Tume
na Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) na
503,193 waliandikishwa na Tume ya
uchaguzi Zanzibar(ZEC)
Hata hivyo
baada ya ya kuhakiki na
uchakataji wa taarifa za wapiga kura Tume
ilibaini kuwa jumla ya
wananchi 231,955 waliandikishwa
zaidi ya mara moja na 3,870 walikuwa sio
Raia wa Tanzania
Alisema Tume
imejipanga kuhakikisha kila mpiga kura mwenye sifa
za kupiga kura anapiga kura yake
siku hiyo ya uchaguzi pasipo kubughudhiwa
Jane aliwaasa
viongozi hao wa vyama vya siasa
wazingatie sheria na taratibu
za uendeshaji wa tatatibu za
uchaguzi na waepuke kutowa lugha
zozote za uchochezi zinazo weza
kuleta uvunjifu wa amani
na kuhatarisha maisha ya
Watanzania
Alifafanua kwamba uzoefu
unaonyesha kwamba katika kampeni zinaendelea pale ambapo
wafuasi wa vyama tofauti wanapokutana
uwezekano wa kutokea vurugu ni
mkubwa na sehemu nyingine vurugu zimetokea na kusababisha maafa,majeruhi na uharibifu wa mali
Hivyo endapo
kila chama kitaamua
kuwaelekeza wafuasi wake
kubaki kwenye vituo vya kupigia kura
upo uwezekano mkubwa wa kutokea
vurugu ambazo zinaweza
kupelekea kuwatia hofu
na kuwasumbua wapiga kura ni mkubwa
hivyo kuhujumu zoezi la upigaji
kura
0 comments:
Post a Comment