Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi
wakiwa na silaha mbili za kivita aina ya
SMG wamewavamia wafanya biashara
wa kununua mpunga katika
Kijiji cha Vikonge Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi na kupola kiasi cha zaidi ya shilingi milioni
saba na simu
Kamanda wa polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari
aliwaambia Wahandishi wa
habari kuwa tukio hilo la upolaji lilitokea hapo
Agosti 16 majira ya saa saba usiku
Kidavashari
alisema siku
hiyo ya tukio majambazi hao wakiwa
na silaha mbili za kivita
aina ya SMG waliwavamia Wafanyabiashara na kufanya
upolaji wa fedha kiasi cha Tsh 7,180,000
na simu mbili zenye thamani ya
Tsh 5,000,000
Katika
tukio hilo Majambazi hao
waliwapola Siasa Simon( Kasumuni ) mkazi
wa Kasulu Kigoma aliyepolwa kiasi cha Tsh 5,000,000 simu moja aina ya Techno
yenye thamani ya shilingi laki
mbili na nusu na kadi ya Benki ya CRDB
Kidavashari
alimtaja mfanyabiashara mwingine
aliyepolwa kuwa ni Edward Filemon(Mnonga) Mkazi wa Kasulu Kigoma alipolwa
Tsh 2,180,000 simu moja aina
ya Techno yenye thamani ya Tsh 250,000 pia alijeruhiwa
baada ya kupigwa malungu katika
mkono wake wa kushoto na
kumsababishia maumivu makali
Kabla ya
tukio hilo wafanyabiashara hao
wawili walikuwa wamefika kijijini hapo
mnamo tarehe 15 Agosti kwa lengo la kununua mpunga
kutoka kwa wakulima wa Kijiji
hicho
Alisema
siku hiyo wakati wakiwa wamelala katika
nyumba waliokuwa wamefikia
Kijijini hapo ya Mnyaga
Maziku ndipo majambazi
hao walipowavamia kwa kuvunja
mlango na kisha waliingia ndani na kufyatua risasi sita
na kisha walifanya uporaji huo
Jeshi la Polisi kupitia kwa raia wema walipata taarifa na kuwahi
katika eneo hilo na baada ya
kufika walishirikiana na Sungsungu wa
eneo hilo ambapo walifuatilia nyayo za majambazi hao hadi kwenye pori la Luhafe na walifanikiwa kuwaona majambazi hao
wakiwa umbali wa mita 150 na kisha walianza kuwakimbiza
Alisema majambazi
hao baada ya kuona karibu wakamatwe waliamua kutupa chini
mfuko wa salphate na kutokomea porini kusiko julikana
Baada ya
upekuzi kufanyika kwenye mfuko huo kulikutwa
na silaha mbili
za kivita aina ya SMG zenye
Namba UA-3379 na 19111685 ikiwa
na risasi 23 pia katika eneo hilo la tukio
yaliweza kupatikana maganda
matatu ya risasi za bunduki
aina ya SAR na SMG
Kamanda
Kidavashari aliwaeleza waandishi wa Habari kuwa jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne ambao bado wanaendelea kushikiwa na
jeshi la Polisi
Aliwataja watuhumiwa hao walikamatwa kuwa ni
Mayunga Saguda (44) Halila Tiga(33) Mnyaga Maziku(30) wakazi wa Kijiji cha Luhafe Wilaya ya Mpanda na Shija
Mahoma (30) Mkazi wa Mtaa wa Kawajense Mjini
Mpanda
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi ameendelea
kuwashukuru Wananchi wanaoendelea kushirikiana
na jeshi la Polisi katika
kufanikisha kudhibiti vitendo vya
uhalifu hasa katika maeneo yaliyombali na jeshi la polisi
0 comments:
Post a Comment