Home » » HOT NEWS: CHADEMA WAMWANDIKIA BARUA YA KUCHUKUA FOMU YA UBUNGE MGOMBEA AMBAE HAKUTEULIWA NA KAMATI KUU

HOT NEWS: CHADEMA WAMWANDIKIA BARUA YA KUCHUKUA FOMU YA UBUNGE MGOMBEA AMBAE HAKUTEULIWA NA KAMATI KUU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter   Mguluchuma
Katavi
Chama cha  Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya  Mlele  Mkoa wa Katavi  kimejikuta kiko kwenye wakati  mgumu baada ya kumwandikia  barua ya  kumtambulisha  kuchukua  fomu za kugombea  Pascal  Mayala kwa msimamizi wa  uchaguzi wa Jimbo la Kavuu kuwa  ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Kavuu wakati  kamati kuu ya Chama hicho imemteuwa na kumtangaza mtu  mwingine  kuwa  ndio   mgombea wa Jimbo la Kavuu
Mayala   ambae  alikuwa ni  mshindi wa  pili  kwenye  kura za maoni   za  chama  hicho  baada ya kushindwa na  Laulent  Mangweshi  alichukua  fomu  hizo  kwa msimamizi wa  uchaguzi wa Jimbo la Kavuu katika  ofisi ya  msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo hilo  iliyoko  Inyonga  Wilaya ya Mlele
Mara baada ya kukabidhi  barua iliyokuwa ikimtambulisha kuwa ni mgombea wa  Jimbo hilo  alianza mara moja kufuata taratibu za ujazazi wa fomu  hizo   na kisha  alikwenda  Mahakamani na kura kiapo
Mgombea  huyo alichukua  fomu ikiwa ni  masaa  machache  kabla ya  kamati kuu ya  chama  hicho  kutangaza  majina ya wagombea Ubunge  kupitia  chama  hicho  huku   kamati kuu ya CHADEMA  ikiwa  imemtangaza Laulent  Mangweshi kuwa ndio  mgombea wao  wa  CHADEMA  wa Jimbo la Kavuu na sio Pascal  Mayala
Katibu wa  CHADEMA  wa  Mkoa wa Katavi   Almasi  Ntije  alieleza kuwa  Viongozi wa  chama  hicho wa  ngazi ya Wilaya walifanya  makosa  kumwandikia  barua ya kumtambulisha kwa msimamizi wa uchaguzi kuwa   Mayala  ndio mgombea wa  chama hicho
Alifafanua kuwa  kamati kuu ya  Chama  hicho  ndiyo yenye  mamlaka  ya kuteuwa wagombea wa nafasi ya Ubunge  kwenye majimbo
Katibu  huyo  alisema    uongozi wa  Chama  hicho unafanya utaratibu  wa kuwasiliana na mwanasheria wao ili waweze kumwandikia  barua  msimamizi wa uchaguzi ili aweze kuondoa  jina la  Pascal  Mayala   kwenye  nafasi ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Kavuu
Mwandishi wa  habari hizi alipomtafuta  Mayala   kwa  njia ya simu yake ya mkononi alieleza kuwa yeye yuko safari akiwa anatokea  mjini  Mpanda kwenda Inyonga  Wilayani  Mlele kwa lengo la kukabidhi fomu za kugombea Ubunge kwa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kavuu Mkoani Katavi

KATAVI YETU BLOG

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa