Tuesday, June 2, 2015

WAKAMATWA NA NYARA ZA SERIKALI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuwakamata  wakiwa na nyara za Serikali  meno mawili ya  ya Kiboko   mkia wa  Twiga na  ngozi ya nyati wakiwa wamehifadhi ndani ya nyumba yao
 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari jana kuwa watuhumiwa hao wawili walikamatwa jana majira ya saa  sita na nusu mchana katika Mtaa wa Kambukaleli  Mjini hapa
Kidavashari aliwataja  watuhumiwa hao wanaoshikiliwa na jeshi la Polisi kuwa ni  Paulo  Masuka(52) na    Juliana  Rogasira (45) wakazi wa Mtaa wa Tambukaleli  mjini  Mpanda
 Alisema  kukamatwa kwa watuhumiwa  kulitokana na  baada ya  polisi  kupata taarifa  kutoka kwa Raia wema  kuwa watuhumiwa  hao  wamehifadhi  nyara hizo za serikali  nyumbani kwao
 Baada ya taarifa hizo kuwa   zimelifikia jeshi la Polisi  walituma   polisi kwenda  nymbani kwa watuhumiwa  kwa lengo la kufanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo
Polisi  walifanikiwa  kufika  katika  nyumba ya watuhumiwa   hao na kuwafanyia upekuzi  na waliweza  kufanikiwa  kuwakamata watuhumiwa  wakiwa na nyara hizo za Serikali wakiwa wamezihifadhi ndani ya nyumba yao
Kamanda Kidavashari alifafanua kuwa thamani ya nyara hizo walizokamatwa nazo watuhumiwa hao wawili thamani yake bado  haija  julikana bado
Na watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani  ili  wakaweze kujibu  tuhuma zao zinazo wakabili

No comments:

Post a Comment