Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Petro
Magawe (40) Mkazi wa Mtaa wa
Ilembo Wilaya ya Mpanda amekutwa
akiwa amejinyonga kwenye mti
kwa kutumia shati lake alilokuwa amevaa
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi kamishina mwandamizi msaidizi
Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari jana kuwa tukio hilo la
kujinyonga kwa mtu huyo lilitokea hapo jana majira ya saa mbili asubuhi katika eneo la ofisi ya mistu katika mtaa wa Majengo A mjini
hapa
Kabla ya tukio hilo marehemu huyo alifika kwenye kituo cha Polisi cha Wilaya ya Mpanda nakueleza
kuwa anaomba na anahitaji awekwe mahabusu
Kamanda Kidavashari alisema kauli hiyo ya marehemu aliyoitowa ya
kuomba awekwe mahabusu iliwashitua
polisi waliokuwa zamu kwani sio jambo la kawaida kwa mtu kuomba awekwe mahabusu
Hivyo
marehemu alipatiwa msaada wa
kupewa PF 3 kwa ajiri ya kwenda
Hospitali kupatiwa matibabu kwani
alionekana kama mtu aliyechanganikiwa
Kamanda Kidavashari alisema baada ya marehemu kuwa amepewa PF 3 alioga kwenye kituo cha polisi kuwa anaelekea
hospitalini
Alieleza
baada ya hapo marehemu alikuja
kuonekana hapo jana majira ya saa kumi
na mbili asubuhi akiwa amejinyonga juu
ya mti kwa kutumia shati lake
Kidavashari alisema chanzo cha tukio hilo bado haki kulikana
na jeshi la polisi
linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo
No comments:
Post a Comment