Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mahakama ya ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemuhukumu kifungo cha miaka 20 jela Mkazi waMtaa wa
Nsemlwa Migazini Mjini Mpanda
EmiliFerix baada ya kupatikanana na kosa
la kukamatwa akiwa na kilo120 za nyamayaKongoni yenye thamaniya
shilingi laki sita
Mshitakiwa alihukumiwa adhabuhiyo hapojuzi
mbele yaHakimu mkazi
mfawidhi wa Mahakama ya Wilayaya MpandaChiganga Ntengwa baada ya mahakama kulidhika na ushahidi
uliotolewa mahakamani hapo wa pande
mbili za mashitaka na utetezi
Awali
katika kesi hiyo mwendesha mashitaka mwanasheria wa Hifadhi ya Taifa Katavi Pele
Malima aliiambia Mahakama kuwa
mshitakiwa Emili alitenda kosa hilo Februari 12 mwaka 2011 majira ya saa nne usiku
Ilidiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka huyo
wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi kuwa siku
hiyo ya tukio Askari wa Hifadhi ya Taifa
ya Katavi walipata taarifa kutoka kwa
raia wema kuwa mshitakiwa amekuwa
akijihusisha na uwindaji haramu katika
hifadhi ya Taifa ya Katavi ndipo walipokwenda kumpekua nyumba kwake na
walifanikiwa kumkamata akiwa na kilo 120
za nyama ya Kongoni
Katika kesi
hiyo upande wa mashitaka ulikuwa na
mashahidi wanne ambapo mshitakiwa hakuwa
nashahidi yoyote naalijitetea mwenyewe
KablayakusomahukumuhiyoHakimuChiganga alimpa
nafasi mshitakiwa ya kuweza kujitetea ilikama
anaweza kuwa na sababu ya msingi
inayoweza kiishawishi mahakama ipunguzie adhabu
Katika utetezi
wake mshitakiwa Emili aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kile alichodai kuwa anaumri mkubwa wa miaka 61 na kuna familia ambayo
inamtegemea
Hata hivyo
utetezi huo ulipingwa vikali na mwendesha mashitaka wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi na aliiomba
mahakama itowe adhabu kali kwa
mshitakiwa kwani tatizo la kukamatwa kwa wawindaji haramu
limekuwa likiongezeka siku hadi siku
hivyo aliomba mahakama itowe adhabu
kali ili iwefundisho kwa
wawindaji haramu haramu
Akisoma hukumu
hiyo Hakimu Chiganga
alieleza kuwa mshitakiwa
amepatikana na kosa
na kuvunja sheria ya kifungu
namba 86(1) (2)
(c) (i) cha sheria ya wanyama
pori namba 5 ya mwaka 2009
Hivyo Mahakama
pasiposhaka lolote imetowa
adhabu kwa mshitakiwa
kutumikia jelakifungo cha miaka
ishirini kuanzia juzi
No comments:
Post a Comment