Wednesday, June 10, 2015

HATARI SANA; AUWAWA KWA KUKATWA MAPANGA BAADA YA KUNYWESHWA POMBE NYINGI YA KIENYEJI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na   Walter  Mguluchuma
Katavi
Jeshi la Polisi  Mkoa wa Katavi linamshikilia  Lugwa  Saimoni ((9)  Mkazi wa Kitongoji cha  Kungwi Wilaya ya Mpanda  kwa tuhuma za kumuuwa  kikatili  Shija   Nyango  (45)  Mkazi wa kitongoji hicho  kwa kumkatakata na panga katika sehemu mbalimbali za mwili wake  baada ya kumnywesha pombe nyingi ya kienyeji aina ya komoni kupita kiasi

Tukio la mauwaji ya kikatili ya mtu huyo  lilitokea hapo juzi majira ya  saa tano  usiku  katia Kitongoji  hicho cha Kungwi kilichopo Wilaya  Mpanda 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia jana waandishi wa Habari  kuwa siku hiyo ya tukio  marehemu   alifiika   kwenye klabu  kinachuza  pombe  ya kienyeji majira ya saa kumi na moja jioni   kinachomilikiwa  na Renatha  Ngomeni  ambae ni shemeji yake na marehemu huyo  kwa lengo la kunywa pombe 

Kidavashari alisema  ilipofika majira ya saa  moja mtuhumiwa  Lugwa    Somoni  alifika kwenye kilabu  hicho walipokuwa  wakiuza  pombe ya kienyeji  aina ya komoni huku akiwa na mwenzake  mmoja  aliyetambulika kwa jina moja la  Lugwa  Mkazi wa Kijiji hicho 

 Alisema watu hao wawili  walijumuika  na marehemu  kunywa nae pombe  huku wakiwa wanaendelea kumnunulia marehemu pombe  mfululizo    hadi majira ya saa tano usiku 

Baada ya kumnywesha pombe marehemu kwa muda mrefu  na watuhumiwa walibaini kuwa  marehemu amelewa  hivyo  waliaga na kuondoka  kwenye kilabu hicho cha pombe  kuwa wanakwenda makwao 

Kamanda Kidavashari alieleza  watuhumiwa hao baada ya muda mfupi walirejea kwenye kilabu hicho cha pombe huku wakiwa wamwshika mapanga mikononi mwao   na kisha waliinza kumshambulia marehemu  ambee walikuta akiwa anaendelea kunywa pombe  kwa kumkata  kata katika sehemu mbali mbali za mwili wake huku marehemu  akiwa anapiga mayowe ya kuomba msaada 

 Alisema pamoja na marehemu  kuwa anapiga mayowe ya kuomba msaada watu hao hawakujari  na waliendelea kumshambulia kwa kumkata na mapanga hadi  marehemu alipofariki Dunia na wao walitokomea 

 Jeshi la  Polisi kwa kushilikiana na wananchi wakitongoji hicho walifanya msako mkali na kufanikiwa kumkamata  mtuhumiwa    Lugwa Saimoni  na bado wanaendelea  kumshikilia kwa mahojiano zaidi 

Kidavashari aliwaambia waandishi  wa Habari kuwa jeshi la Polisi bado  linaendelea na msako wa  kumsaka mtuhumiwa mwingine  aliyejulikana kwa jina la Lugwa  mkazi wa  Kiitongoji hicho ambae walishilikiana na mtuhumiwa aliyekamatwa kufanya mauwaji hayo 

Mtuhumiwa  Lugwa Saimoni  anatarajiwa kufikishwa Mahakamani  mara baada ya uchunguzi utakapo kuwa umekamilika ili ajibu mtuhuma zinazo mkabili  na chanzo cha   tukio hilo bado  hakijajulikana

No comments:

Post a Comment