Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mahakama ya
Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi
imemuhukumu kifungo cha miaka 30 jela
Atanazi Julias(30) Mkazi
wa Mjini hapa
baada ya kupatikana na hatia ya
kumbaka kwa nguvu msichana(23)
mkazi wa mtaa wa Mji mwema
mjini Mpanda
Atanazi
Juliasi Mkazi wa
Mtaa wa Kotazi Mjini hapa
alihukumiwa hukumu hiyo
jana mbele ya
Hakimu Mkazi wa
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Odila
Amworo baada ya mahakama
kulidhika na ushahidi uliotolewa Mahakamani
hapo na mara baada kutolewa
hukumu hiyo mshitakiwa alianguka na kupoteza fahamu kwa muda
Awali
katika kesi hiyo mwendesha
mashitaka Mkaguzi msaidizi wa
Polisi Godfrey Ndangala
aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa huyo alitenda
kosa hilo hapo
januari 30 mwaka huu majira ya saa sita mchana katika mtaa wa Mji mwema mjini hapa nyumbani kwao na msichana aliyebakwa
Ilidaiwa
Mahakamani hapo kuwa siku
hiyo ya tukio mshitakiwa
alifika nyumbani kwao na
msichana huyo na hakuweza kuwakuta wazazi wa msichana
huyo
Mwendesha mashitaka
Ndangala aliiambia mahakama
kuwa mshitakiwa alifika mida
hiyo nyumbani kwa msichana huyo
baada ya kujua wazazi wake wote mida
hiyo huwa wanakuwa hawapo nyumbani
wanakuwa kwenye shughuli zao za
biashara
Alisema baada ya mshitakiwa kuwa
amefika nyumbani hapo
alimwomba msichana huyo apatie maji maji ya kunywa kwani
anasikia kiu na ndio shida iliyompeleka
hapo
Alieleza
mshitakiwa alikubaliwa ombi lake
la kupewa ya kunywa na ndipo
msichana huyo alipoingia ndani na
kuchukua maji ya kunywa na
wakati akipewa maji hayo ghafla mshitakiwa alimshika
msichana huyo na kuanza kumbaka
licha ya mwanamke huyo kupiga
kelele za kuomba msaada
mshitakiwa hakujali na aliendelea
kumbaka
Katika utetezi
wake mshitakiwa aliomba
mahakama imwachie huru kwani
hakutenda kosa hilo na pia imwonee
huruma kwani umri wake bado ni
mdogo
Utetezi huo
ulipigwa vikali na mwendesha
mashitaka ambae alidai kuwa
vitendo vya ubakaji vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku
katika Mkoa wa Katavi hivyo ni
vema Mahakama itatowa adhabu
kali kwa mshitakiwa
iliiwefundisho kwa watu wengine
wenye tabia kama hiyo ya mshitakiwa
Hakimu Odila Amworo akisoma
huku hiyo aliieleza
kuwa mahakama baada ya kusikiliza kesi hiyo kwa upande wa mashitaka na utetezi mahakama imelidhika na ushahidi uliotolewa wa mpande washita
Hivyo
Mahakama imemtia hatiani mshitakiwa
Atanazi Julias i na
imemtia hatiani kwa kifungu
cha sheria No 130( 1) a na kifungu cha
sheria 131(1) cha kanuni ya
adhabu sura ya 16 marekebisho ya mwaka 2002 hivyo mshitakiwa
amekuhumiwa kutumikia jela kifungo cha
miaka 30 jela
Baada ya hakimu
kusoma hukumu hiyo
mshitakiwa alianguka ghafla na
kupoteza fahamu kutona na mshituko wa adhabu hiyo hata hivyo
baada ya muda alipata fahamu na kisha
alipelekwa kwenye gereza la Mpanda kwa ajiri ya kutumikia kifungo hicho cha
miaka 30
No comments:
Post a Comment