Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowasaa amepata wadhamini 3,450 Mkoani Katavi walomdhamini fomu za kugombea Urais kupitia CCM kwa ajiri ya uchaguzi ujao
Lowassa aliwasiri jana mchana akitokea Mkoani Kigoma ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kuzungukia mikoani kutafuta wadhamini wa kumdhamini ili kugombea Urais kupitia CCM
Lowassa aliwasiri uwanja wa ndege wa Mpanda majira ya saa 6.33 mchana ambapo alipokewa na umati mkubwa wa wananchi wa mji wa Mpanda na mamia ya waendesha pikipiki ambao waloongoza msafara na kuelekea ofisi ya CCM ya Mkoa wa Katavi iliyoko katika mtaa wa Kasimba huku umati mkubwa wa watu wakiwa wamejipanga pembezoni mwa barabara
Baada ya msafara wake huo kutoka kwenye ofisi za CCM mkoa ulielekea kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Mpanda ambapo kulikuwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa na shauku ya kumsikiliza
Katibu wa CCM wa Wilaya ya Mpanda Elizebeth Kashili alieleza kuwa jumla ya wana CCM 3,450 wamejaza fomu za kumdhami ni Edward Lowassa
Alifafanu kuwa katika fomu ya kwanza jumla ya wanachama 45 wa CCM wamemdhamini kwenye fomu hiyo na fomu ya pili jumla ya wanachama 3,405 na tano wamemdhami ni kwenye fomu hiyo
Kwa upande wake Lowassa aliwashukuru wana CCM waliojitokeza kwa wingi katika kumdhamini kwenye fomu hizo na aliwashukuru wananchi wa mji wa Mpanda kwa mapokezi makubwa waliomfanyia ambayo yeye aliyaita ni mapokezi ya aina yake
Pia aliwataka wananchi wa Mkoa wa Katavi waliojiandikisha kwenye daftari la kupiga kura wahakikishe wanavilinda vitambulisho vyao kwani ndivyo vitakavyo wasaidia wakati wa kupiga kura na wajiepuke na watu watakao taka kuwashawishi kununua vitambulisho vyao
Hata hivyo haweza kuwaendelea kuwahutubia wananchi hao waliokuwa na shauku ya kumsikiliza kutokana na kile alichodai kuwa chama kimeisha wakataza wagombea wote kutozungumza lolote kwa sasa
No comments:
Post a Comment