Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Waziri Mkuu
Mizengo Pinda juzi amepokewa na umati mkubwa wa wananchi wa
Mji wa Mpanda
huku wakiwa na mabango yaliondikwa Pinda
Kimya kimya hadi
Ikulu na wengine wakiwa na matrekita
wakiashilia kuwa ni mtoto wa mkulima na msafara mkubwa wa pikipiki na
maagari
Pinda aliwasiri juzi jioni
akitokea Mkoani Dodoma
ikiwa ni wa ziara
ya kwanza kuzungukia mikoani kutafuta
wadhamini wa kumdhamini ili kugombea
Urais kupitia CCM ikiwa
ni baada ya masaa machache
baada ya mgombea mwingine Edward
Lowaassa kuwa ameondoka mjini hapa na kuelekea Mkoani Rukwa
Pinda aliwasiri
uwanja wa ndege wa Mpanda majira ya saa
12 na dakika 20 jioni ambapo alipokewa na umati
mkubwa wa wananchi wa mji wa
Mpanda ambao walikuwa wamejipanga barabarani kuanzia saa nane mchana
walioanzia uwanja wa ndege wa
Mpanda hadi nyumbani
kwake katika mtaa wa
Makanyagio
Msafara wa
Pinda ulianza kuanzia
uwanja wa ndege wa Mpanda
huku ukiwa umeongozwa
na mamia ya waendesha pikipiki
na msafara mkubwa wa
magari na watembea kwa miguu wakipita kwenye mitaa ya
Kashaulili Majengo A na Majengo
B na kisha msafara ulifika nyumbani
kwake katika mtaa wa Makanyagio
Msafara huo ulikutana na wakati
mguu kutokana na umati
mkubwa wa watu waliokuwa wamejitokeza huku wakiimba nyimbo zinazo sema Pinda Rais huku
wakiwa wanapeperusha kanga vitenge mashati na majani
Kutokana
na hari hiyo walinzi wake Pinda
walilazimika kufanya kazi ya ziada
ambapo walinzi wake wawili walilazimika
kung’ing’ia kwenye milango
miwili ya kulia na kushoto ya
gari alilokuwa amepanda
Pinda
Pinda
alitarajiwa jana kwenda Inyonga
Wilaya ya Mlele ambako ni
jimboni kwake kwa ajiri ya kutafuta wadhamini wa kumdhamini fomu za kugombea Urais kupia CCM katika uchaguzi wa
mwaka huu
Naleo jumanne
anatarajiwa kudhamini na wanachama wa
CCM wa Wilaya ya
Mpanda katika ofisi za CCM Wilaya
ya Mpanda
No comments:
Post a Comment