Home » » PINDA WASILI KATAVI KTAFUTA WADHAMINI APOKEWA NA MABANGO TREKITA MAMIA YA PIKIPIKI NA MAELFU YA WATU‏

PINDA WASILI KATAVI KTAFUTA WADHAMINI APOKEWA NA MABANGO TREKITA MAMIA YA PIKIPIKI NA MAELFU YA WATU‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na  Walter  Mguluchuma 
Katavi
Waziri  Mkuu    Mizengo Pinda  juzi amepokewa  na umati mkubwa wa  wananchi  wa  Mji   wa   Mpanda   huku  wakiwa na  mabango yaliondikwa  Pinda  Kimya  kimya  hadi  Ikulu  na wengine wakiwa na  matrekita   wakiashilia kuwa ni  mtoto wa  mkulima na msafara mkubwa wa pikipiki na maagari
 Pinda   aliwasiri juzi   jioni      akitokea  Mkoani  Dodoma   ikiwa ni   wa ziara  ya kwanza kuzungukia  mikoani  kutafuta  wadhamini  wa kumdhamini  ili kugombea  Urais  kupitia  CCM ikiwa  ni  baada ya masaa  machache  baada ya mgombea  mwingine  Edward  Lowaassa  kuwa  ameondoka mjini hapa na kuelekea  Mkoani Rukwa
 Pinda  aliwasiri  uwanja wa  ndege wa Mpanda  majira ya saa  12 na  dakika 20  jioni  ambapo alipokewa na  umati  mkubwa wa  wananchi wa mji wa Mpanda    ambao walikuwa wamejipanga  barabarani kuanzia saa nane   mchana  walioanzia  uwanja wa  ndege wa  Mpanda  hadi  nyumbani  kwake  katika  mtaa wa  Makanyagio     
 Msafara wa  Pinda  ulianza  kuanzia  uwanja wa  ndege wa   Mpanda  huku  ukiwa  umeongozwa  na  mamia ya waendesha  pikipiki  na  msafara  mkubwa wa  magari  na  watembea kwa miguu wakipita kwenye mitaa ya Kashaulili Majengo  A na  Majengo  B na kisha  msafara ulifika   nyumbani  kwake  katika mtaa wa  Makanyagio  
 Msafara huo ulikutana  na wakati  mguu  kutokana  na umati  mkubwa wa  watu  waliokuwa wamejitokeza huku wakiimba  nyimbo zinazo sema Pinda  Rais huku  wakiwa wanapeperusha  kanga  vitenge mashati na majani
 Kutokana  na hari hiyo walinzi wake  Pinda walilazimika kufanya  kazi ya ziada ambapo walinzi wake wawili walilazimika  kung’ing’ia  kwenye  milango  miwili ya  kulia na kushoto  ya  gari  alilokuwa  amepanda  Pinda
 Pinda  alitarajiwa  jana kwenda  Inyonga  Wilaya ya Mlele  ambako ni jimboni  kwake kwa ajiri ya  kutafuta wadhamini wa kumdhamini  fomu za kugombea Urais kupia CCM katika  uchaguzi wa  mwaka huu
 Naleo jumanne  anatarajiwa    kudhamini na  wanachama wa  CCM  wa  Wilaya ya  Mpanda  katika ofisi za  CCM Wilaya  ya  Mpanda 


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa