Monday, June 15, 2015

JUST IN: PINDA APATA WADHAMINI ZAIDI YA 4,000 ASEMA RAIS AJAE ANAMJUA MUNGU TUU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma 
Katavi
Waziri Mkuu  Mizengo  Pinda  amepata wadhamini  zaidi ya 4,000 Mkoani    Katavi ambao wamadhamini  fomu za kugombea   Urais kupia  CCM  kwa ajiri ya  kugomea urais  katika uchaguzi mkuu ujao na  alisema kuwa  Rais ajae  anae mjua ni Mungu  peke yake hata wagombea wakiwa zaidi ya 30
 Pinda  ambae  yupo kwenye  ziara ya kutembelea Mikoa  mbalimbali  kwa ajiri ya kutafuta wadhami wa kumdhamini fomu za kugombea Urais  alidhamini   hapo  jana
Katibu  wa  CCM  wa  Wilaya ya  Mpanda    Elizabeth  Kashamili aliwaeleza  maelfu ya wakazi wa  mji wa  Mpanda  waliokuwa  wamekusanyika  kwenye  ofisi za CCM  Wilaya ya  mpanda kwa lengo la  kushuhidia  tendo  Pinda kukabidhi  fomu za kugombea Urais alizodhaminiwa na wanachama wa CCM wa Mkoa wa katavi ambapo  alieleza kuwa jumla ya wanachama 4243 wamedhamini Pinda kwenye fomu hizo
Katibu  huyo alifafanua kuwa  Wilaya ya Mlele  Pinda amedhaminiwa na wanachama  1440 na Wilaya ya Mpanda amedhaminiwa na wanachama wa CCM  2803
Kwa upande   wake Pinda aliwshukuru wanachama  waliojitokeza kwa wingi kwenye kumdhamini fomu hizo kwenye mbio za kumpata mgombea kupia  chama hicho
Alisema hata wagombea wakiwa zaidi ya 30 wanaogombea  lakini Mungu peke yake ndio   anae jua ni nani atakae kuwa Rais  ajae  wa  Nchi  yetu
    uzuri wa jambo hilihakuna  mtu  atakae  kuwa anajua  Rais  ajae   hivyo  lazima  watu  waombe  sana   kwa  Mungu  kwani yote ndiye  anayepanga  alisema Pinda  na kushangiliwa na umati huo
 Pia  alichukua nafasi hiyo kuwashukuru wananchi wa mji wa Mpanda kwa mapokezi makubwa waliomfanyia  juzi wakati alipo wasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda na kufananisha mapokezi hayo kuwa yalikuwa ni yakihistoria  Katika Mkoa wa Katavi na kusema kama ni mvua basi ilikuwa ni mvua ya mawe
Pinda alisema  kumbe hakua amekosea kunzia  ziara yake ya  kutafuta wadhamini  katika  Mkoa wa Katavi kwani amefarijika sana jinsi alivyo pokewa na  ametiwa moyo mno   na wanachi wa Mkoa wa Katavi  katika kuugombea Urais
 Aliwashauri wakazi wa Mkoa wa Katavi kujitokeza kwa wingi  kuwapokea wagombea wengine watakao pita   Mkoani  hapa ni  vizuri  mkawapokea na kuwasikiliza na kuwaona
 Pinda aliwaeleza wananchi hao kuwa    baada ya kumaliza ziara yake jana  Mkoani  Katavi  ataanza ziara  leo katika  Mkoa wa Rukwa kisha  ataelekea Mikoa ya Mbeya  Niombe , Iringa  na  Songe

No comments:

Post a Comment