Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Jeshi la Polisi
Mkoa wa Katavi linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuwakamata wakiwa na nyara za Serikali meno mawili ya ya Kiboko
mkia wa Twiga na ngozi ya nyati wakiwa wamehifadhi ndani ya
nyumba yao
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri
Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari jana kuwa watuhumiwa hao wawili
walikamatwa jana majira ya saa sita na
nusu mchana katika Mtaa wa Kambukaleli
Mjini hapa
Kidavashari
aliwataja watuhumiwa hao wanaoshikiliwa
na jeshi la Polisi kuwa ni Paulo Masuka(52) na Juliana
Rogasira (45) wakazi wa Mtaa wa Tambukaleli mjini
Mpanda
Alisema
kukamatwa kwa watuhumiwa kulitokana na baada ya
polisi kupata taarifa kutoka kwa Raia wema kuwa watuhumiwa hao
wamehifadhi nyara hizo za
serikali nyumbani kwao
Baada ya taarifa hizo kuwa zimelifikia jeshi la Polisi walituma
polisi kwenda nymbani kwa
watuhumiwa kwa lengo la kufanya
uchunguzi juu ya tuhuma hizo
Polisi walifanikiwa
kufika katika nyumba ya watuhumiwa hao na kuwafanyia upekuzi na waliweza
kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa na nyara hizo za Serikali wakiwa
wamezihifadhi ndani ya nyumba yao
Kamanda
Kidavashari alifafanua kuwa thamani ya nyara hizo walizokamatwa nazo watuhumiwa
hao wawili thamani yake bado haija julikana bado
Na watuhumiwa hao
wanatarajiwa kufikishwa mahakamani
ili wakaweze kujibu tuhuma zao zinazo wakabili
0 comments:
Post a Comment