Home » » HOT NEWS: MWANDISHI WA HABARI MAARUFU WA GAZETI LA THE GUARDIAN GELARD ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE

HOT NEWS: MWANDISHI WA HABARI MAARUFU WA GAZETI LA THE GUARDIAN GELARD ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mwandishi wa habari wa gazeti la Guardian  Gelard  Kitabu akiwa  katika Ofisi za CHADEMA  jimbo la Nsimbo   zilizopo  katika Kijiji  cha  Songambele   Tarafa ya Nsimbo  Wilaya ya Mlele muda mfupi kabla hajachukua fomu za kugombea ubunge (CHADEMA) wa jimbo la Nsimbo hapo juzi
Picha na Walter  Mguluchuma-Katavi yetu Blog
 Msafara wa bodaboda wakiongoza maandamano  ya kumsindikiza  mwandishi wa habari wa Guardian  Gelard Kitabu kuchukua fomu za kugombea ubunge (CHADEMA) wa jimbo la Nsimbo hapo juzi Picha na Walter  Mguluchuma


Na   Walter  Mguluchuma
Katavi
Mwandishi  maaarufu  hapa  Nchini wa  gazeti la Guardian    Gelard Kitabu  amechukua  fomu za kugombea  ubunge wa Jimbo   la  Nsimbo   Mkoa wa Katavi  kupitia  cha  Chadema  kwa ajiri  ya kupitishwa na  chama hicho  katika uchaguzi  Mkuu wa oktoba   mwaka huu
Kitabu  ambae ni mshindi wa tuzo ya uhandishi  wa habaari  za SADC ambayo hutolewa  kwa waandishi  bora  wa kuandika  habari za maendeleo  na mazingira  katika nchi  za jumuia  ya kusini mwa  Afrika  alichukua fomu  hizo juzi  katika  Kijiji chaSongambele   Tarafa ya  Nsimbo  Wilaya ya Mlele  Mkoani  hapa
Mwandishi  huyo mbali ya  kushinda  tuzo  ya SADC  pia Kitabu  hivi  karibuni  alishinda  tuzo  mbili  kubwa katika  nafasi ya kwanza  moja ikiwa ni TANAPA 2013  na  nyingine  ya  baraza la habari Tanzania (MCT) 2014 katika  kipemgele cha mazingira
Iwapo  atapita  kwenye kura za maoni za( CHADEMA ) mwandishi  huyo  mwandamizi  wa habari  atapeperusha  bendera  ya  chama hicho  kugombea na mgombea wa CCM katika uchaguzi mkuu utakao fanyika mwezi oktoba  
 Akizungumza   na wachama wa chama hicho pamoja na  mamia  ya  wananchi wa Tarafa ya Nsimbo waliokuwa wamekusanyika hapo  alisema wakati umefika  wa yeye  kuwahudumia  wanachi wa jimbo  hilo la  Nsimbo
Alisema jimbo hilo  limekuwa nyuma  kimaendelea  hivyo wakati umefika sasa  wa jimbo  hilo  kumpata Mbunge  atakae liongoza  ambae ni yeye Kitabu
Nimejipima  na nimetazama  hali halasi ya maendeleo  na  kero za huduma za jamii kuwa ni mbovu na rasilimali nyingi za Mkoa huu wa Katavi hazisimamiwi ipasavyo  hivyo nimeona  nijitose  kwenye uchaguzi  ujao  alisema Gelard Kitabu
 Alisema uamuzi wake  pia umetokana na shinikizo   kutoka kwa  wananchi  wa jimbo hilo  kumtaka achukue fomu
Nimesukumwa na  makundi  ya wananchi   wangu wazee ,wanawake , na vijana  na  nimedhamilia  kuleta maendeleo kwa wananchi wa Jimbo la Nsimbo na Mkoa wa Katavi kwa ujumla alisema Kitabu
 Alisema  endapo  atapitishwa na chama chake  ataweka mipango  ambayo  itawasaidia wananchi  kuondokana na umasikini ,kupambana na rushwa  na wizi  wa fedha za wananchi  za miradi ya maendeleo  kama maji ,elimu , barabara  ujenzi wa  zahanati na  vituo vya afya
 Alieleza  atasimamia  suala la rasrimali  zilizipo  katika  Mkoa wa Katavi kwa kuhakikisha rasrimali zilizopo zinawanufaisha wananchi wote wa Mkoa wa Katavi
Wanachi wa makundi mbali mbali walimchangia na kumkabidhi jumla ya kiasi cha shilingi laki nne kwa ajiri ya kulipia fomu za kugombea ubunge
Kitabu  atakuwa ni  mwandishi  wa  habari wa kwanza kuweka  historia  ya mgombea ubunge kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Katavi kwani hakuna mwandishi wa habari aliwahi kugombea nafasi hiyo katika  Mkoa wa Katavi
Na Katavi yetu Blog


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa