Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Picha na Walter Mguluchuma-Katavi yetu Blog
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mwandishi maaarufu
hapa Nchini wa gazeti la Guardian Gelard Kitabu
amechukua fomu za kugombea ubunge wa Jimbo la
Nsimbo Mkoa wa Katavi kupitia
cha Chadema kwa ajiri
ya kupitishwa na chama hicho katika uchaguzi Mkuu wa oktoba mwaka huu
Kitabu ambae ni mshindi wa tuzo ya uhandishi wa habaari
za SADC ambayo hutolewa kwa
waandishi bora wa kuandika
habari za maendeleo na
mazingira katika nchi za jumuia
ya kusini mwa Afrika alichukua fomu hizo juzi
katika Kijiji chaSongambele Tarafa ya
Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoani
hapa
Mwandishi huyo mbali ya
kushinda tuzo ya SADC pia Kitabu
hivi karibuni alishinda
tuzo mbili kubwa katika
nafasi ya kwanza moja ikiwa ni
TANAPA 2013 na nyingine
ya baraza la habari Tanzania
(MCT) 2014 katika kipemgele cha
mazingira
Iwapo atapita
kwenye kura za maoni za( CHADEMA ) mwandishi huyo
mwandamizi wa habari atapeperusha
bendera ya chama hicho
kugombea na mgombea wa CCM katika uchaguzi mkuu utakao fanyika mwezi oktoba
Akizungumza
na wachama wa chama hicho pamoja na
mamia ya wananchi wa Tarafa ya Nsimbo waliokuwa
wamekusanyika hapo alisema wakati
umefika wa yeye kuwahudumia
wanachi wa jimbo hilo la Nsimbo
Alisema jimbo
hilo limekuwa nyuma kimaendelea
hivyo wakati umefika sasa wa
jimbo hilo kumpata Mbunge atakae liongoza ambae ni yeye Kitabu
Nimejipima na nimetazama hali halasi ya maendeleo na
kero za huduma za jamii kuwa ni mbovu na rasilimali nyingi za Mkoa huu
wa Katavi hazisimamiwi ipasavyo hivyo
nimeona nijitose kwenye uchaguzi ujao
alisema Gelard Kitabu
Alisema uamuzi wake pia umetokana na shinikizo kutoka kwa
wananchi wa jimbo hilo kumtaka achukue fomu
Nimesukumwa
na makundi ya wananchi
wangu wazee ,wanawake , na vijana
na nimedhamilia kuleta maendeleo kwa wananchi wa Jimbo la
Nsimbo na Mkoa wa Katavi kwa ujumla alisema Kitabu
Alisema
endapo atapitishwa na chama
chake ataweka mipango ambayo
itawasaidia wananchi kuondokana
na umasikini ,kupambana na rushwa na
wizi wa fedha za wananchi za miradi ya maendeleo kama maji ,elimu , barabara ujenzi wa
zahanati na vituo vya afya
Alieleza
atasimamia suala la
rasrimali zilizipo katika
Mkoa wa Katavi kwa kuhakikisha rasrimali zilizopo zinawanufaisha
wananchi wote wa Mkoa wa Katavi
Wanachi wa
makundi mbali mbali walimchangia na kumkabidhi jumla ya kiasi cha shilingi laki
nne kwa ajiri ya kulipia fomu za kugombea ubunge
Kitabu atakuwa ni mwandishi
wa habari wa kwanza kuweka historia
ya mgombea ubunge kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Katavi kwani hakuna
mwandishi wa habari aliwahi kugombea nafasi hiyo katika Mkoa wa Katavi
Na Katavi yetu Blog
No comments:
Post a Comment