Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Kiongozi Mkuu wa chama
cha ACT wazalendo Zito
Kabwe amesema kwamba viongozi
wa wanaongoza vyama vya siasa hata
nchini sio lazima watoke
sehemu moja kama
ambavyo baadhi ya vyama vya siasa vinavyo fanya
Kauli hiyo aliitowa hapo jana wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mji wa Mpanda katika
mkutano wa hadhara uliofanyika
katika uwanja wa shule ya Msingi Kashaulili mjini
hapa
Zito alisema kumekuwa
na tabia ya vyama vya siasa
kutaka viongozi wa ngazi za juu
kutoka katika Mkoa moja au kanda moja na mapokeo yake anapo tokea mtu
mwingine kutoka mkoa mwingine au kanda nyingine hujengewa chuki na kuondolewa ndani ya chama
Alieleza ACT wamuamua funya ziara
katika Mkoa wa Katavi kwa lengo
la kukitambulisha rasmi chama hicho kwa
wananchi wa Mkoa wa Katavi
Alifafanua wapo baadhi ya viongozi wa vyama vya viasa kazi
yao kubwa ni kupiga kele tuu lakini
hawana uwezo wa kujenga hoja za msingi
kwa wananchi hivyo ni budi
wananchi wakachambua pumba ni zipi na mchele ni upi
Naomba kiongozi hata moja wa CHADEMA
anieleze ni hoja ipi ambayo
aliwahi kutowa na ikasabisha hata
Mtendaji wa kata akafukuzwa
kazi yeye anaamini
hakuna kiongozi hata moja wa CHADEMA aliwahi kujenga hoja hiyo alisema zito
Kabwe na kushangiliwa na wananchi
pia alizungumzia sakata
lake na sababu kubwa iliyomfanya afukuzwe kwa kuvuliwa
nyadhifa zake na uanachama kwenye chama
cha CHADEMA wakati alipokuwa naibu katibu
mkuu Tanzania Bara
Alisema sakata lake la lilianzia toka
mwaka 2012 wakati akiwa
ni mwenyekiti wa kamati ya bunge
ya ukaguzi wa fedha za Serikali
Alifafanua baada ya kuona matumizi fedha hayaendi vizuri kwenye vyama
vya siasa vilivyokuwa vinapewa
ruzuku ya fedha kutoka serikali alimwagiza mkaguzi mkuu wa serikali avifanyie ukaguzi vyama vyote
vinavyopokea ruzuku kutoka Serikali jinsi vinavyo tumia ruzuku hiyo
Zito
alisema baada ya kutowa maagizo
hayo aliitwa na kamati kuu ya
CHADEMA na alihojiwa ni kwani amaamua
kafanya hivyo kabla ya kukitonya kwanza
chama chake
Alieleza kuwa baada ya kuulizwa
hivyo na wajumbe wa kamati kuu aliwajibu
kuwa yeye anachoangalia
ni utaifa kwanza mambo mengine
kwake huya yanafuata hivyo
aliamua kutowa maagizo hayo kwa manufaa
ya Taifa sio kwa manufaa ya vyama
Alisema baada ya kuwa wanajua hawamuwezi kwenye maswala ya kujibu hoja ndipo walipoamua
kumuondoa kwa njia nyingine waliokuwa wanaijua wapo
Kwaupanda wake msanii marufu hapa
nchini Afende Sele
aliwataka wakazi wa Mkoa wa Katavi kutoshabikia mambo ya siasa kama ambavyo wanavyoshabikia timu za mpira
Mkutano huo ambao ulikuwa na watu wengi ulikuwa na ulinzi mkali wa askari polisi ambao walikuwa na sare za jeshi hilo na wasio kuwa na sere kufuatia taarifa
ambazo zilikuwa zimeenea kabla ya mkutano huo kuanza kuwa kuna kundi
linalodaiwa kuwa ni la wafuasi wa
CHADEMA walikuwa wamepanga kumzomea Zito wakati akihutubia lakini hari hiyo
haikutokea
No comments:
Post a Comment