Home » » HATARI SANA: MWANAMKE ALBINO AKATWA MKONO KISHA WATU HAO KUTOKOMEA NA KIGANJA CHAKE KUSIKO JULIKANA.

HATARI SANA: MWANAMKE ALBINO AKATWA MKONO KISHA WATU HAO KUTOKOMEA NA KIGANJA CHAKE KUSIKO JULIKANA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi-yetu blog
Mwanamke mmoja mwenye ulemavu wa ngozi(Alubino)   Remi  Luchoma(30)  Mkazi kIjiji  cha  mwamachoma   Kata  ya Mamba Wilaya ya Mlele  Mkoa wa Katavi  amekatwa mkono wake wa kushoto na kisha watu hao wametokomea na kiganja cha mkono wake na amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa ajiri ya kupatiwa matibabu
Kaimu  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda Dr  Joseph Mkemwa  alisema  kuwa  tukio la kukatwa  mkono  kwa Alubino huyo lilitokea hapo jana majira ya saa sita usiku nyumbani kwa wazazi wake katika Kijiji hicho
 Alisema baada ya kukatwa kiganja chake cha mkono wa kushoto  Alubino huyo alipelekwa katika kituo cha afya cha Mamba ambapo alipewa rufaa na  kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa ajiri ya matibabu zaidi
Dr Msemwa alieleza kuwa  Remi  Luchoma amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda katika wodi  namba mbili akiwa anapatiwa matibabu huku hari yake ikiwa inaendelea vizuri
Kwa upande wake  Masuma Luchuma  ambae  ni kaka wa Alubino huyo  alieleza kuwa  tukio hilo la kukatwa kiganja cha mkono  wa dada yake  kilitokea kwenye chumba alichokuwa akiishi Alubino huyo mwenye watoto wanne
 Alisema  siku hiyo ya tukio majira ya saa sita usiku  alisikia  watu wakivunja mlango  wa chumba alichokuwa amelala    Remi  na kisha  baada ya muda mfupi alisikia dada yake huyo Alubino akipiga mayowe ya kuomba msada
 Alieleza  alijihitahidi  kufanya jitihada za kutoka nje ili kumwokoa Alubino alikini alishindwa kutoka  kutokana na watu hao  kuwa wamemfungia mlango wake kwa nje
 Alisema  hari hiyo ilimfanya apige kengele ya jembe kama ishara ya kuomba msada kwa majirani  hari ambayo iliwafanya watu hao watokomee kusiko julikana
Nae  mwanamke huyo mwenye  ulemavu wa ngozi   Remi  Luchoma  akiongea kwa uchungu mkubwa  huku akiwa amelazwa  hospitalini  alisema kuwa  yeye alikuwa amelala ndani ya chumba chake na ndipo watu wawili asio wafahamu  walivunja mlango wa  chumba chake na  kuingia  ndani huku wakiwa wameshika panga  mkononi
  Alisema  ndipo watu hao  walipoingia ndani walimkata kiganja cha mkono wake wa kushoto hari ambayoilimfanya apate maumivu makali na kisha watu hao walitokomea na kiganja cha mkono huo mahari kusiko julikana
Kwa upande wake mama mdogo wa Alubino huyo  Maliselina  Jackisoni  alisema kuwa  wakati  Remi  alipokuwa akipiga  mayowe  aliamka na alipochungulia dirishani aliwaona watu hao wawili ambao  hakuwa akiwafahamu  wakitoka kwenye chumba cha Remi huku wakiwa wameshika kiganja cha mkono wake hari ambayo ilimlazimu na yeye kupiga mayowe ya kuomba msaada
 Alisema Remi  kutoka na milango yao kuwa imefungwa kwa nje alishindwa kutoka nje hadi walipofunguliwa milango yao na Remi ambae muda huo alikuwa akivuja damu nyingi kutokana na kukatwa kwa kiganja cha mkono wake
 Alieleza majirani walifika kwenye eneo hilo na kisha walikwenda kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi cha Majimoto na polisi walifika kwenye eneo hilo baada ya muda mfupi na walianza jitihada za kuwatafuta watu hao
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema polisi wanaendelea na msako mkali wa kuwasaka watu waliohusika na tukio hilo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa