Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi-yetu blog
Mwanamke mmoja
mwenye ulemavu wa ngozi(Alubino)
Remi Luchoma(30) Mkazi kIjiji
cha mwamachoma Kata
ya Mamba Wilaya ya Mlele Mkoa wa
Katavi amekatwa mkono wake wa kushoto na
kisha watu hao wametokomea na kiganja cha mkono wake na amelazwa katika Hospitali
ya Wilaya ya Mpanda kwa ajiri ya kupatiwa matibabu
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda
Dr Joseph Mkemwa alisema
kuwa tukio la kukatwa mkono
kwa Alubino huyo lilitokea hapo jana majira ya saa sita usiku nyumbani
kwa wazazi wake katika Kijiji hicho
Alisema baada ya kukatwa kiganja chake cha
mkono wa kushoto Alubino huyo alipelekwa
katika kituo cha afya cha Mamba ambapo alipewa rufaa na kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya
Mpanda kwa ajiri ya matibabu zaidi
Dr Msemwa alieleza
kuwa Remi Luchoma amelazwa katika Hospitali ya Wilaya
ya Mpanda katika wodi namba mbili akiwa
anapatiwa matibabu huku hari yake ikiwa inaendelea vizuri
Kwa upande
wake Masuma Luchuma ambae
ni kaka wa Alubino huyo alieleza
kuwa tukio hilo la kukatwa kiganja cha
mkono wa dada yake kilitokea kwenye chumba alichokuwa akiishi
Alubino huyo mwenye watoto wanne
Alisema
siku hiyo ya tukio majira ya saa sita usiku alisikia
watu wakivunja mlango wa chumba
alichokuwa amelala Remi na kisha
baada ya muda mfupi alisikia dada yake huyo Alubino akipiga mayowe ya
kuomba msada
Alieleza
alijihitahidi kufanya jitihada za
kutoka nje ili kumwokoa Alubino alikini alishindwa kutoka kutokana na watu hao kuwa wamemfungia mlango wake kwa nje
Alisema
hari hiyo ilimfanya apige kengele ya jembe kama ishara ya kuomba msada
kwa majirani hari ambayo iliwafanya watu
hao watokomee kusiko julikana
Nae mwanamke huyo mwenye ulemavu wa ngozi Remi
Luchoma akiongea kwa uchungu
mkubwa huku akiwa amelazwa hospitalini
alisema kuwa yeye alikuwa amelala
ndani ya chumba chake na ndipo watu wawili asio wafahamu walivunja mlango wa chumba chake na kuingia
ndani huku wakiwa wameshika panga
mkononi
Alisema
ndipo watu hao walipoingia ndani
walimkata kiganja cha mkono wake wa kushoto hari ambayoilimfanya apate maumivu
makali na kisha watu hao walitokomea na kiganja cha mkono huo mahari kusiko
julikana
Kwa upande wake
mama mdogo wa Alubino huyo
Maliselina Jackisoni alisema kuwa
wakati Remi alipokuwa akipiga mayowe aliamka na alipochungulia dirishani aliwaona
watu hao wawili ambao hakuwa
akiwafahamu wakitoka kwenye chumba cha
Remi huku wakiwa wameshika kiganja cha mkono wake hari ambayo ilimlazimu na
yeye kupiga mayowe ya kuomba msaada
Alisema Remi
kutoka na milango yao kuwa imefungwa kwa nje alishindwa kutoka nje hadi
walipofunguliwa milango yao na Remi ambae muda huo alikuwa akivuja damu nyingi
kutokana na kukatwa kwa kiganja cha mkono wake
Alieleza majirani walifika kwenye eneo hilo na
kisha walikwenda kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi cha Majimoto na polisi
walifika kwenye eneo hilo baada ya muda mfupi na walianza jitihada za
kuwatafuta watu hao
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema polisi wanaendelea na msako mkali
wa kuwasaka watu waliohusika na tukio hilo
No comments:
Post a Comment