Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Watu watatu wakazi wa Makazi ya Wakimbizi ya
Katumba Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi
wanashikiliwa na jeshi la Polisi
Mkoa wa Katavi kwa tuhuma
za kuwakamata wakiwa na vipande vitatu vya meno ya
Tembo vyenye uzito wa
kiligramu nane yenye thamani ya
zaidi ya shilingi milioni kumi na
moja
Watuhumiwa hao waliokamatwa na meno hayo ya
Tembo ni Frank Hamisi(18) Steven
Jonas (22) wakazi wa Kijiji cha Mnyaki A Makazi ya Wakimbizi ya Katumba na Jackson
Erasto (34) Mkazi wa kijiji cha
Ivungwe Makazi ya Wakimbizi ya Katumba
Wilaya ya Mlele
Kamanda wa Jeshi
la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari
aliwaambia waandishi wa habari
kuwa watuhumiwa hao walikamatwa jana
majira ya saa tatu asubuhi
katika eneo la kijiji cha
Mnyaki A katika makazi ya wakimbizi ya Katumba
Alisema watuhumiwa hao walikamatwa kufutia taarifa zilizokuwa zimelifikia jeshi
la Polisi kutoka kwa Raia wema kuwa
katika eneo la Kijiji cha Mnyaki
A kwenye chumba alichopangishwa mwanafunzi
wa kidato cha nne wa shule ya
Sekondari ya Katumba aitwaye Evos John(19) kwenye nyumba
inayomilikiwa na Felix Gado
kuna meno ya tembo yalikuwa yamehifadhiwa na watuhumiwa kwa ajiri ya kuyasafirisha kwa Treani kutoka Katumba kuyapela Tabora
Alieleza
kufuatia taarifa hizo ndipo Polisi
walipochukua hatua za haraka
za kwenda kwenye eneo la Kijiji
hicho cha Mnyaki A na kuizingira nyumba hiyo
waliokuwa wameitilia mashaka
Kidavashari alieleza
ndipo upekuzi ulifanyika
kwenye nyumba hiyo na
viliweza kupatikana vipande vitatu vya meno ya Tembo yenye uzito wa kilogramu nane vyevye thamani ya Tsh 11,250,000 vikiwa ndani ya chumba walikuwa wamelala watuhumiwa hao
vikiwavimefungashwa tayari kwa
kusafirishwa
Katika uchunguzi wa awali umebaini
kuwa watuhumiwa kabla ya tukio la kukamatwa walikuwa wameomba kulala
katika chumba cha mwanafunzi Eno John kwa lengo la kusubilia usafiri wa Treni ya kutoka Mpanda kuelekea Tabora
Kamanda
Kidavashari aliwaeleza waandishi wa habari kuwa
wanafunzi huyo aliwaruhusu watuhumiwa kulala kwenye chumba chake kwani walikuw a wakifahamiana nao
kutokana na mahusiano ya kindugu
na hivyo yeye siku hiyo aliamua kuwaachia chumba chake
na alikwenda kulala kwa
mwanafunzi mwenzake jirani na hapo
Mpaka sasa watuhumiwa hao waliokamatwa
wanaendelea kushikiliwa na jeshi la
polisi na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya
upelelezi utakapo kuwa
umekamilika
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi ametowa wito
kwa jamii kuachana na tabia
ya kujihusisha na biashara haramu
ya nyara za Serikali kwani kufanya
hivyo ni kinyume cha sheria
No comments:
Post a Comment