Home » » HALMASHAURI ZA SHAURI KUTENGA MAENEO YA MARISHO YA MIFUGO

HALMASHAURI ZA SHAURI KUTENGA MAENEO YA MARISHO YA MIFUGO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
 Halmashauri za Wilaya  za  Mkoa wa Katavi  na vijiji vyote vya Mkoa wa Katavi  zimeshauriwa  kutenga  maeneo kwa ajiri ya marisho ya mifugo  ili kuondoa  migogoro  ya wakulima  na wafugaji 
Ushauri huo umetolewa hapo jana na Mwenyekiti wa chama cha wafugaji (CCWT)   wa  wa Mkoa wa Katavi Mussa Kabushi  wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa  Habari ofisini kwake mjini hapa
Alisema hivi karibuni alifanya ziara  ya kutembelea  maeneo  ya Halmashauri zote   Mkoani hapa  na aliweza kubaini kwenye ziara  hiyo   kuwa   hakuna maeneo yoyote  yaliotengwa  na Halmashauri   kwenye vijiji  kwa ajiri ya marisho  ya mifugo
Ndio maana  wafugaji  wa maeneo  mengi  wamekuwa wakilazimika  kuchungia mifugo  kwenye maeneo  yaliotengwa  kwa  matumizi  mengine  ambayo  sio rasmi  kwa mifugo na kusababisha migogoro   alisema   Kabushi
 Alisema  anaziomba  Halmashauri  zote za  Mkoa wa Katavi  zikubaliane na ushauri  wa chama cha wafugaji cha  Mkoa wa Katavi   kwa kutenga  maeneo ya kutosha  kwa wafugaji  kwani wafugaji  wakotayari   kuchangia  mapato  kutokana na  mifugo  yao
Alifafanua  Halmashauri ambayo  itatenga  maeneo ya kutosha  yenye ewezo wa  kukaa ng’ombe wa kutosha itakuwa imejiongezea mapato yake kwani wafugaji wamekubaliana kuwa watakuwa  wanalipa  ushuru  kiasi cha   tsh 5'000  kwa kila ng’ombe  na Halmashauri  itakuwa inapata tsh  2,000 kwa kila ng’ombe  na tsh  3'000 zitakuwa zinakwenda kwenye chama cha wafugaji kwa ajiri ya shughuli za kupanda nyasi na kuchimba malambo ya maji
 Alifafanua kwa kiasi hicho cha fedha endapo Halmashauri kwenye eneo lake itakuwa na  ng’ombe  laki  tatu itaweza kujipatia  ushuru wa kiasi cha shilingi milioni mia sita kwa mwaka kutoka na ushuru wa mifugo hiyo
Pia  alisema Halmashauri  ziwe na utaratibu  wa kutowa elimu  kwa wafugaji  itakayo  wawezesha  wafugaji  kuitambua  mipaka  ya hifadhi  za Taifa  .vyanzo vya maji  sambamba  na  utunzaji wa mazingira  na  kudhibiti  ukataji wa miti  holela
 Wafugaji wa kutoka mikoa ya Tabora ,Mwanza ,Shinyanga na Simiyu wamekuwa wakiingia kwa wingi  Mkoani  Katavi kotokana na Mkoa huu kuwa  na maeneo mengi ya adhi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa