Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Halmashauri za Wilaya za
Mkoa wa Katavi na vijiji vyote
vya Mkoa wa Katavi zimeshauriwa kutenga
maeneo kwa ajiri ya marisho ya mifugo
ili kuondoa migogoro ya wakulima
na wafugaji
Ushauri huo
umetolewa hapo jana na Mwenyekiti wa chama cha wafugaji (CCWT) wa wa
Mkoa wa Katavi Mussa Kabushi wakati
alipokuwa akizungumza na waandishi wa
Habari ofisini kwake mjini hapa
Alisema hivi
karibuni alifanya ziara ya
kutembelea maeneo ya Halmashauri zote Mkoani
hapa na aliweza kubaini kwenye ziara hiyo kuwa
hakuna maeneo yoyote
yaliotengwa na Halmashauri kwenye
vijiji kwa ajiri ya marisho ya mifugo
Ndio maana wafugaji
wa maeneo mengi wamekuwa wakilazimika kuchungia mifugo kwenye maeneo
yaliotengwa kwa matumizi
mengine ambayo sio rasmi
kwa mifugo na kusababisha migogoro alisema
Kabushi
Alisema
anaziomba Halmashauri zote za
Mkoa wa Katavi zikubaliane na
ushauri wa chama cha wafugaji cha Mkoa wa Katavi kwa kutenga
maeneo ya kutosha kwa wafugaji kwani wafugaji wakotayari kuchangia
mapato kutokana na mifugo
yao
Alifafanua Halmashauri ambayo itatenga maeneo ya kutosha yenye ewezo wa kukaa ng’ombe wa kutosha itakuwa imejiongezea
mapato yake kwani wafugaji wamekubaliana kuwa watakuwa wanalipa
ushuru kiasi cha tsh 5'000
kwa kila ng’ombe na
Halmashauri itakuwa inapata tsh 2,000 kwa kila ng’ombe na tsh
3'000 zitakuwa zinakwenda kwenye chama cha wafugaji kwa ajiri ya
shughuli za kupanda nyasi na kuchimba malambo ya maji
Alifafanua kwa kiasi hicho cha fedha endapo
Halmashauri kwenye eneo lake itakuwa na
ng’ombe laki tatu itaweza kujipatia ushuru wa kiasi cha shilingi milioni mia sita
kwa mwaka kutoka na ushuru wa mifugo hiyo
Pia alisema Halmashauri ziwe na utaratibu wa kutowa elimu kwa wafugaji itakayo
wawezesha wafugaji kuitambua
mipaka ya hifadhi za Taifa
.vyanzo vya maji sambamba na
utunzaji wa mazingira na kudhibiti
ukataji wa miti holela
Wafugaji wa kutoka mikoa ya Tabora ,Mwanza
,Shinyanga na Simiyu wamekuwa wakiingia kwa wingi Mkoani
Katavi kotokana na Mkoa huu kuwa
na maeneo mengi ya adhi
No comments:
Post a Comment