Sunday, May 24, 2015

HII NI ZAIDI YA HATARI: WANANDOA WAWILI WAUWAWA KIKATILI KWA KUCHINJWA SHINGO ZAO NA KUTENGANISHWA NA KIWILIWILI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na  Walter  Mguluchuma
Katavi yetu blog
Watu  wawili wa  familia  moja  Mke na Mume  wakazi wa Kitongoji cha Makambo  Kata ya Itenka Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wameuwawa kikatili kwa kuchinjwa shingo zao na  kutenganishwa na kiwiliwili  wakati wakiwa wamelele ndani ya nyumba yao na watu wasiofahamika
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  aliwataja wanandoa hao wawili waliouwawa kikatili kuwa ni  Seth Mwakalimbwa (65) na Yakoba  Kalulu(48)  wakazi wa kitongoji hicho
Kidavashari aliwaambia jana waandishi wa habari kuwa tukio hilo la mauwaji ya kikatili lilitokea hapo juzi majira ya  usiku  nyumbani kwa wanandoa hao waliokuwa wakiishi pamoja kama mke na mume
 Alisema kwamba  marehemu  hawa  wakati wa uhai wao walikuwa  wakiishi  kwenye nyumba  yao  huku  wakiwa p eke yao  pasipo kuwa na  watu wengine kwenye nyumba hiyo waliishi kwa muda mrefu
 Ilipo fika juzi  asubuhi  balozi wa eneo hilo aitwaye  Wilbroad Mahenge  ambae  ni jirani ya marehemu  hao  aliingiwa na mashaka  baada ya kutowaona  wanandoa hao wawili kwa kipindi cha siku mbili mfululizo
 Kamanda Kidavashari alieleza  balozi huyo  kutokana na kutowaona  wanandoa hao  aliamua  kufika  katika makazi yao    na alipofika hapo  alikuta  mirango ya nyumba yao aliikuwa iko wazi hari ambayo ilimfanya apate mashaka zaidi
 Alisema alijaribu kuwaita kwa majina yao lakini hakuna  aliyeweza kuitika   na aliamua  kuingia ndani  ya nyumba  yao  na  ndipo  aliwakuta wakiwa  wamelazwa kitandani  huku   wakiwa wamefariki dunia kwa kuchinjwa shingo zao na kutenganishwa na kiwiliwili
 Baada ya kuona hari hiyo balozi  Wilbroad  alitoka nje na kasha alikwenda kutowa taarifa kwenye uwongozi wa Serikali ya Kitongoji ambao na wao walitowa taatifa kwa jeshi la polisi ambao walifika kwenye eneo hilo baada ya muda mfupi
Kamanda Kidavashari alisema  chanzo cha  tukio la mauwaji hayo ya kikatili  linahusishwa  na imani  za  kishirikina  na mpaka sasa  hakuna mtu  wala watu  waliokamatwa  kuhusika na tukio hilo
 Aidha  jeshi la polisi kwa kushirikiana  na uongozi  na wanakijiji  cha  Makambo  wanaendelea  na msako  ili  kuweza  kuwabaini  wale  watu  wote  waliohusika  katika mauwaji ya wanandoa hao

No comments:

Post a Comment