Na Walter
Mguluchuma
Katavi yetu blog
Serikali inatarajia kujenga barabara kwa kiwango cha rami barabara za Mkoa wa Katavi ilikuuunganisha Mkoa huo na mikoa inayopakana nayo ili kuufanya Mkoa huo kuwa kituo kikubwa cha wafanyabiashara wa ndani ya Nchi na nje ya nchi
Kauli hiyo ilitolewa hapo jana na Waziri wa Ujenzi Dr John Magufuli wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mji wa Mpanda kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Mpanda
Alisema kwa kipindi cha miaka mitano ijayo Mkoa wa Katavi barabara zake zinazounganishwa na mikoa mingine haitakuwa na barabara ambayo itakuwa inaunganishwa na Mkoa mwingine ambayo itakuwa na kiwango cha barabara ya udongo
Alieleza kuwa yeye kama Waziri wa Ujenzi ataendelea kusimamia kwa karibu miradi yote ya ujenzi wa barabarazikiwemo za Mkoa wa Katavi kama ambavyo Serikali ilivyo ahaidi kwa wananchi ili hata hapo atakapo kufa aweze kuchaguliwa huko mbinguni kuwa waziri wa Ujenzi wa malaika wanaoishi mbinguni
Alifafanua kuwa gharama ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha rami ni kubwa kwani kilometa moja ya ujenzi wa barabara ya rami inagharimu kiasi cha shilingi milioni 1000(BILIONI MOJA)
Dr Magufuli alisema pamoja na gharama hizo kubwa Serikai bado imeendelea na ujenzi wa kutengeneza barabara kwa kiwango cha rami kwa kuwa inatambua kuwa asilimia 99.3 ya watanzania wanatumia usafiri wa barabara
Alisema wakati wa uhuru mwaka 1961 nchi yetu ilikuwa na barabara zilizojengwa kwa rami zilikuwa ni kilometa 1330 wakati huu wa kipindi cha Serikali ya awamu ya nne kuna jumla ya kimometa 11,154 zimetengenezwa kwa kiwango cha rami
Alieleza babara ya kutoka Mpanda kwenda Ipole Mkoani Tabora yenye urefu wa kilometa 359 inatarajiwa kuanza kujengwa kwa kiwango cha rami mwaka huu kutokana na fedha za ufadhili wa Benki ya Afrika na tenda ya kumpata mkandarasi itatangazwa hivi karibuni baada ya taratibu kuwa zimekamilika
Barabara ya Sumbawanga kuelekea Mpanda Mkoani Katavi inaendelea kujengwa kwa kiwango cha rami kwa fedha za makusanyo ya ndani kazi hiyo ya ujenzi inafanywa na makampuni matatu ya Kichina
Alisema Serikali inaendelea na kutafuta fedha kwa ajiri ya kutengeneza barabara kwa kiwango cha rami kutoka Mpanda kwenda Uvinza Mkoani Kigoma ilikukamilisha kuziunganisha barabara zote za mkoa wa Katavi
Dr Magufuli alieleza mpaka sasa ni mikoa miwili ambayo haijaunganishwa na mikoa inayopakana nayo kwa barabara za kiwango cha rami ambayo mikoa hiyo ni Katavi na Njombe
Alifafanua hadhima ya Serikali mara baada ya kupata uhuru ilikuwa ni kuiunganisha mikoa yote ya Tanzania kwa barabara za kiwango cha rami
Awali kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambae ni mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima katika taarifa aliyoisoma mbele ya Waziri wa ujenzi John Magufuli alieleza kuwa Mkoa wa Katavi una jumla ya kilometa 1,101.46 za barabara zinazohudumiwa na wakala wa barabara wa Mikoa TANROADS kati ya hizo kilometa 474.3 ni barabara kuu na kilometa 627.16 ni barabara za Mkoa
mwisho

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment