Home » » KATAVI KUUNGANISHWA NA MIKOA MINGINE KWA BARABARA ZA RAMI MAGUFULI ATAMANI KWENDA KUWA WAZIRI WA UJENZI WA MALAIKA MBINGUNI‏

KATAVI KUUNGANISHWA NA MIKOA MINGINE KWA BARABARA ZA RAMI MAGUFULI ATAMANI KWENDA KUWA WAZIRI WA UJENZI WA MALAIKA MBINGUNI‏



Na  Walter  Mguluchuma
Katavi yetu blog
Serikali  inatarajia     kujenga  barabara   kwa kiwango  cha  rami    barabara  za  Mkoa wa Katavi ilikuuunganisha  Mkoa huo  na  mikoa inayopakana nayo ili kuufanya Mkoa huo kuwa kituo  kikubwa cha wafanyabiashara wa ndani ya Nchi na nje ya nchi  
Kauli hiyo  ilitolewa hapo jana na Waziri  wa Ujenzi  Dr  John  Magufuli wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mji wa Mpanda kwenye  mkutano wa hadhara  uliofanyika kwenye   uwanja wa shule ya msingi Mpanda
  Alisema kwa kipindi cha miaka mitano ijayo  Mkoa wa Katavi  barabara zake  zinazounganishwa   na mikoa  mingine  haitakuwa na  barabara  ambayo itakuwa inaunganishwa   na Mkoa mwingine  ambayo  itakuwa  na kiwango cha barabara  ya udongo
Alieleza kuwa yeye kama Waziri wa Ujenzi  ataendelea  kusimamia kwa karibu miradi yote ya ujenzi wa barabarazikiwemo za  Mkoa wa Katavi   kama ambavyo Serikali ilivyo ahaidi kwa wananchi  ili hata hapo atakapo kufa  aweze  kuchaguliwa huko mbinguni  kuwa waziri wa Ujenzi wa malaika wanaoishi mbinguni   
 Alifafanua kuwa  gharama ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha rami ni  kubwa  kwani kilometa moja ya ujenzi wa barabara ya rami inagharimu  kiasi cha shilingi milioni 1000(BILIONI MOJA)
 Dr Magufuli alisema  pamoja na gharama hizo kubwa Serikai  bado imeendelea na ujenzi wa kutengeneza  barabara kwa kiwango cha rami  kwa kuwa inatambua kuwa  asilimia 99.3 ya watanzania  wanatumia usafiri wa barabara
Alisema wakati wa uhuru  mwaka 1961 nchi yetu ilikuwa na barabara zilizojengwa kwa rami zilikuwa  ni kilometa 1330 wakati huu  wa kipindi cha Serikali ya awamu ya nne kuna jumla ya  kimometa  11,154 zimetengenezwa kwa kiwango cha rami
 Alieleza  babara ya kutoka Mpanda  kwenda Ipole Mkoani Tabora yenye urefu  wa kilometa  359 inatarajiwa kuanza kujengwa kwa kiwango cha rami  mwaka huu  kutokana na fedha za ufadhili wa Benki ya Afrika   na tenda ya kumpata mkandarasi itatangazwa hivi karibuni  baada ya taratibu kuwa zimekamilika
 Barabara ya Sumbawanga  kuelekea Mpanda Mkoani Katavi inaendelea kujengwa kwa kiwango cha rami  kwa fedha za  makusanyo ya ndani   kazi  hiyo  ya ujenzi inafanywa na makampuni matatu ya Kichina
 Alisema Serikali  inaendelea na kutafuta fedha  kwa ajiri ya kutengeneza barabara kwa kiwango cha rami kutoka Mpanda kwenda Uvinza Mkoani Kigoma  ilikukamilisha kuziunganisha barabara zote za  mkoa  wa Katavi  
Dr  Magufuli alieleza  mpaka sasa ni mikoa miwili ambayo haijaunganishwa na mikoa inayopakana nayo  kwa barabara za kiwango cha rami ambayo mikoa hiyo ni Katavi na Njombe
Alifafanua  hadhima ya Serikali mara baada ya kupata uhuru ilikuwa ni kuiunganisha mikoa yote ya Tanzania kwa barabara za kiwango cha rami
Awali  kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi  ambae ni  mkuu wa Wilaya ya Mpanda  Paza Mwamlima  katika taarifa aliyoisoma mbele ya Waziri wa ujenzi John  Magufuli  alieleza kuwa  Mkoa wa  Katavi  una jumla ya  kilometa  1,101.46 za barabara  zinazohudumiwa  na wakala wa barabara  wa Mikoa  TANROADS kati ya hizo  kilometa  474.3 ni barabara kuu na kilometa  627.16 ni barabara za  Mkoa
mwisho
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa