Na Walter
Mguluchuma
Katavi yetu blog
Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Dr Ibrahimu Msengi amewataka
Wakurugenzi watendaji na maafisa Elimu
wa Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi kuwa na utaratibu wa kukutana na waalimu
ili kuwasililiza matatizo yao yanayowabili
Waalimu
Dr Msengi alitowa wito huo hapo juzi wakati
alipokuwa akizungumza na waalimu wa
shule za misingi na Sekondari walioko kwenye makazi ya Wakimbizi ya Mishamo kwenye mkutano uliofanyika katika shule ya
Sekondari ya Mishamo wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa majengo ya maabara kwenye Sekondari
ya Mishamo
Alisema nilazima Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri na maafisa
elimu watengeneze mfumo ambao
utawafanya waweze kuwa wanakutana na
waalimu na kuwasikiliza matatizo yao
Alifafanua tabia ya viongozi kutokutana na waalimu na kuwasikiliza kumewafanya waalimu kutumia muda mwingi kwenda kwenye ofisi za
Halmashauri kufuatilia madai yao
mbalimbali
Alisema
hari hiyo imekuwa ikiwafanya
waalimu kutumia muda mchache
kuwafundisha wanafunzi kutona na kutumia muda mwingi kufuatilia madai yao
Pia alieleza Halmashauri
waandae mfumo utakao wafanya waalimu wahudumiwe
mapema iliwawze kurudi mapema
kwenye shule zao na kuwafundisha masomo
wanafunzi
Dr
Msengi alieleza endapo waalimu
watahudumiwa shida zao na mapema
itawafanya waendelee kuwa na moyo wa kufanya kazi zaidi kutokana na wao kuonawanathaminiwa
Alisema itashangaa kuona mwalimu inashindwa kuhudumiwa kwa wakati wakati
maafisa Elimu na wao ni waalimu wenzao na matatizo ya waalimu
wanayafahamu hivyo hawapaswi kusahau waliko toka na watambue kuwa maafisa Elimu
na wao ni waalimu
Aidha kuhusu
matatizo ya nyumba za waalimu alisema Mkoa
unaandaa utaratibu wa kuanzisha mfuko maalumu kwa ajiri ya ujenzi
wa nyumba za waalimu kwa kuwashilikisha
wadau mbalimbali mbapo kila mwaka
watakuwa wanaweza kujenga nyumba mbili
za waalimu kila shule kwa kila mwaka
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment