Thursday, February 5, 2015

CHANGAMOTO ZA KUHARIBIKA KWA BARABARA NI SHIDAA KWA MAENDELEO KATAVI.


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi yetu blog
Mkoa wa Katavi  unakabiliwa na changamoto kubwa  la  kuwa  na barabara  za udongo  ambazo huharibika  kipindi cha  masika  na kusababisha  usumbufu  mkubwa  kwa wakazi  wa Mkoa huo
 Hayo yalielezwa hapo juzi na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima wakati alikuwa  akisoma taarifa ya sekta ya Barabara ya Mkoa wa Katavi mbele ya Waziri wa ujenzi Dr John Magufuli kwenye  mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Mpada mjini hapa
 Alisema  mtandao wa barabara  katika Mkoa wa  Katavi  bado  hauko  imara  kwani  barabara nyingi za Mkoa wa Katavi  ni za shangalawe na udongo  ambazo huaribika  mara  kwa mara  hasa kipindi  cha masika
 Alifafanua  kuwa Mkoa wa Katavi  unajumla ya  kilmeta  1,101.46 za barabara  zinazohudumiwa  na wakala wa  Barabara  wa  Mkoa TANROADS kati ya hizo  kilometa 473.3 ni barabara  kuu na kilometa  627 .16 ni barabara za  Mikoa
 Hata hivyo  kupitia wakala wa  barabara  Mkoa wa Katavi  hadi sasa  angalau  kuna barabara  mbili zinazojengwa  kwa kiwango cha rami
Barabara hizo alizitaja kuwa ni  barabara  ya  Kateto  kwenda Kibaoni  yenye  urefu wa kilometa 20.27 na barabara  ya Sitalike  kwenda Mpanda  yenye  urefu  wa kilometa 36.90
 Alisema  Mkoa  unatarajia  kuipa  kipaumbele  Mikoa ya  pembezoni  mwa nchi  ukiwemo Mkoa wa Katavi  ilikuweza  kurahisisha  huduma  za maendeleo  kwa kuiunganisha  na Mikoa  mingine  kwa barabara  bora za lami
 Muelekeo wa Mkoa wa Katavi sasa ni kuelekea katika uchumi wa Nishati  ya mafuta na Gesi  na utafiti  unaendelea Ziwa Tanganyika  hivyo suala la  mtandao wa bora wa  barabara za  lami  ndani ya Mkoa  na Mikoa ya jirani  linatakiwa kupewa kipaumbele  cha hari ya juu  kwani  kuufungua mkoa wa Katavi  ni kuifungua Tanzania  na  kanda nzima ya Maziwa  Makuu  ikiwemo  nchi ya  DRC Congo
 Kwa upande wake Dr John Magufuli  alieleza kuwa  Serikali  inatajia kumpatia kiasi cha shilingi Bilioni 1.3 mkandarasi anaetengeneza barabara ya lami  Sitalike Mpanda  iliaweze kumaizia ujenzi wa barabara hiyo  ambayo tayari kilomete 26 zimekamilika
Mkandarasi anaetengeneza  barabara ya Kateto  kwenda Kibaoni  hari ya ujenzi wa barabara hiyo inayojengwa na kampuni ya Kichina  bado  hairidhishi  na ametakiwa amalize ujenzi wa barabara hiyo kwa muda alipangiwa vinginevyo atafutiwa mkataba wake alisema Dr Magufuli
 Alieleza Serikali itatoa kiasi cha  shilingi milioni  600 kwa ajiri ya matengenezo ya baraba kwa kiwango cha changalawe  kutoka sitalike kwenda kibaoni yenye urefu wa kilometa 70 pia  Serikali inatarajia kuzipatia Halmashauri za Mji wa Mpanda na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kiasi cha shilingi Bilioni 1.6 kwa ujenzi wa barabara za Halmashauri hiyo

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

No comments:

Post a Comment