CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Katavi,
kimekamilisha safu ya uongozi wake baada ya kupata viongozi wapya
katika uchaguzi uliyofanyika hivi karibuni.
Katika uchaguzi huo uliyosimamiwa na Christopher Nyamwanji, nafasi ya Mwenyekiti ilikwenda kwa Laurant Sanga.
Aidha, Nyamwanji alimtangaza Almas Ntije kuwa Katibu ambaye alikuwa mgombea pekee.
Kwa upande Bavicha, Francis Sylvester alishinda uenyekiti huku upande
wa Baraza la Wazee Mwenyekiti akishinda Milambo Ntamila na Bawacha ni
Irene Lupembe.
Kwa upande wa Wilaya ya Mpanda, Mwenyekiti aliibuka Abrahamu Mapunda
huku Katibu ni Idd Faraji, wakati Mjumbe wa mkutano mkuu taifa
alishinda Nassor Arfi.
Kwa upande wa Wilaya ya Mlele, Mwenyekiti alishinda Augustino Nsokolo
ambaye alikuwa mgombea pekee, wakati Katibu ni Sebastian Kasinge huku
mjumbe wa mkutano mkuu akiibuka Samweli Mpate.
Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment