Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Halmashauri ya
mji wa Mpanda Mkoani Katavi imeanza kutekeleza agizo la
Baraza la Madiwani la Mji huo
lililoitaka Halmashauri hiyo irudishe fedha kiasi cha shilingi
milioni 100 za miradi ya maendeleo ambazo walizitumia kwa matumizi
mengine tofauti na ilivyokuwa imekusudiwa
Haya yalielezwa hapo jana kwenye kikao cha
Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo na kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa
Mpanda Fredinand Filimbi kwenye kikao cha Baraza la Madiwani
kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo
Filimbi
alitowa maelezo hayo wakati alipokuwa ajibu swali la Diwani wa Kata ya Ilembo
Wencesios Kaputa aliyetaka
kufahamu utekelezaji wa agizo la Baraza la Madiwani walilolitowa kwenye
kikao kilichofanyika Septemba 26 mwaka huu
Kwenye kikao
hicho Baraza la madiwani liliingiza
Halmashauri hiyo kurejesha fedha kiasi cha shilingi milioni 100 zilizotolewa na
Serikali kwa ajiri ya miradi ya maendeleo
katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2012 na 2013 lakini fedha hizo hazikutumika kwenye
miradi husika na kupelekea Halmashauri ya Mji wa Mpanda kupata hati
yenye mashaka
Kwenye baraza la madiwani la Septemba 26 baraza hilo
lilimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Mji wa Mpanda ahakakikishe kuwa fedha
hizo shilingi milioni 100 zilizotumika kwa
matumizi yasiyo kusudiwa
zirejeshwe kupitia vyanzo vya mapato ya ndani kwa awamu nne hadi ifikiapo June 30 mwakani
Pia Baraza la
Madiwani liliagiza watumishi
walioshiriki kwenye mchakato wa kuidhinisha fedha hizo za miradi ya maendeleo kwa matumizi
mengine wachukuliwe hatua
za kinidhamu
N a kwa watumishi
ambao Halmashauri haina mamlaka
ya kuwachukulia hatua za
kinidhamu taarifa zao ziwasilishwe ofisi
ya Waziri Mkuu TAMISEMI kwa ajiri ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu
Kaimu Mkurugenzi
wa Halmashauri Ferdinand Filimbi
alilieleza Baraza hilo la madiwani kuwa
tayari wameisha anza kutekeleza
agizo hilo kwani Halmashauri hiyo imerejesha fedha kwa awamu ya kwanza Tsh 25,000,000 kwenye miradi ya
maendeleo kwa stakabadhi Na 99227 ya tarehe 29 Septemba mwaka huu
Kwa upande wa watumishi agizo
limetekelezwa ambapo hatua za kinidhamu zinaendelea kuchukuliwa kwa watumishi ambao Halmashauri inayo mamlaka nayo kwa kuzingatia sheria za Umma Na 18
ya mwaka 2007 na kanuni za utumishi wa umma
ya mwaka 2005 kanuni Na 36
Kwa mtumishi
ambae Halmashauri haina mamlaka
ya kumchukulia hatua za kinidhamu
Halmashauri tayari
imewasilisha kwa katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi barua yenye
Kumb KTV. MTC,S.10,2.81 ya tarehe
22 septemba 2014 kwa kuzingatia sheria za utumishi wa Umma ya mwaka
2002 kifungu cha 5(a)(iii)
Matumizi ya fedha
hizo zilitumika wakati Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo alikuwa ni Joseph
Mchina ambae kwa sasa ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Siginda
na Mkurugenzi wa sasa wa Seleman Lukanga
No comments:
Post a Comment