Home » » HALMASHAURI YA MJI WA MPANDA YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA MADIWANI LA KUREJESHA MILIONI 100

HALMASHAURI YA MJI WA MPANDA YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA MADIWANI LA KUREJESHA MILIONI 100

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Halmashauri ya mji  wa Mpanda  Mkoani Katavi imeanza kutekeleza agizo la Baraza la Madiwani la Mji huo  lililoitaka Halmashauri hiyo irudishe fedha kiasi cha  shilingi  milioni  100  za miradi ya maendeleo ambazo walizitumia  kwa matumizi  mengine   tofauti  na ilivyokuwa imekusudiwa
 Haya yalielezwa hapo jana kwenye kikao cha Baraza la  Madiwani wa Halmashauri hiyo   na kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda  Fredinand Filimbi  kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo
Filimbi alitowa  maelezo hayo  wakati alipokuwa ajibu  swali la Diwani  wa  Kata  ya Ilembo   Wencesios Kaputa aliyetaka kufahamu utekelezaji wa agizo la Baraza la Madiwani walilolitowa kwenye kikao  kilichofanyika Septemba  26 mwaka huu
Kwenye kikao hicho Baraza la madiwani  liliingiza Halmashauri hiyo kurejesha fedha kiasi cha shilingi milioni 100 zilizotolewa na Serikali kwa ajiri ya miradi ya maendeleo  katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2012  na 2013 lakini fedha hizo hazikutumika kwenye miradi husika  na kupelekea  Halmashauri ya Mji wa Mpanda kupata hati yenye mashaka
Kwenye  baraza la madiwani la Septemba 26 baraza hilo lilimwagiza  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda ahakakikishe  kuwa fedha hizo  shilingi milioni 100 zilizotumika  kwa  matumizi yasiyo kusudiwa  zirejeshwe kupitia  vyanzo  vya mapato ya ndani kwa awamu nne  hadi ifikiapo June 30 mwakani
Pia Baraza la Madiwani liliagiza  watumishi walioshiriki  kwenye mchakato  wa kuidhinisha fedha  hizo za miradi ya maendeleo kwa matumizi mengine  wachukuliwe  hatua  za kinidhamu
N a  kwa watumishi  ambao Halmashauri haina mamlaka  ya kuwachukulia hatua  za kinidhamu taarifa zao ziwasilishwe ofisi  ya Waziri Mkuu TAMISEMI kwa ajiri ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Ferdinand Filimbi  alilieleza Baraza hilo la madiwani kuwa  tayari wameisha  anza kutekeleza agizo hilo  kwani Halmashauri hiyo  imerejesha  fedha  kwa awamu ya kwanza  Tsh 25,000,000 kwenye miradi ya maendeleo  kwa stakabadhi  Na 99227 ya tarehe  29 Septemba mwaka huu
  Kwa upande wa watumishi  agizo  limetekelezwa  ambapo  hatua za kinidhamu  zinaendelea kuchukuliwa  kwa watumishi ambao  Halmashauri inayo mamlaka nayo  kwa kuzingatia sheria za Umma  Na  18 ya mwaka 2007 na kanuni  za utumishi  wa umma  ya mwaka 2005 kanuni Na 36
Kwa  mtumishi  ambae Halmashauri  haina mamlaka ya kumchukulia hatua za kinidhamu  Halmashauri  tayari imewasilisha  kwa katibu   Tawala wa Mkoa wa Katavi barua  yenye  Kumb KTV. MTC,S.10,2.81 ya  tarehe 22  septemba  2014 kwa kuzingatia  sheria za utumishi wa Umma  ya mwaka  2002 kifungu cha 5(a)(iii)
Matumizi ya fedha hizo zilitumika wakati Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo alikuwa ni Joseph Mchina  ambae  kwa sasa ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Siginda na Mkurugenzi  wa sasa wa  Seleman Lukanga

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa