Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Wanafunzi wa
Shule ya Msingi Kabulonge iliyoko katika makazi ya Wakimbizi ya Katumba
Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi
wamelalamikia shida wanayo pata waalimu wao ya kutembea umbali wa
kilometa nne kwa ajiri ya kutafuta huduma ya maji kutokana
na shule hiyo kutokuwa na huduma ya maji
Kilio hicho cha
wanafunzi wa Shule hiyo kilitolewa hapo jana kwenye risarayao walioisoma mbele ya mgeni rasmi
mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wakulima wenyeviwanda wakulima na
wafugaji wa Mkoa wa Katavi Hassanal Shabir Dala wakati wa mahafari 32 ya darasa la saba yalifanyika shuleni hapo
Katika risala
hiyo ilisomwa na mwanafunzi Odilia
Eliazek walieleza kuwa shule hiyo
ya Kabulonge i ilianzishwa toka mwaka
1974 lakini haijawahi kuwa na huduma ya
maji shuleni hapo
Walisema toka shule hiyo ilipo anzishwa imekuwa
haina huduma ya maji hari inayosababisha waalimu wao kutembea umbali wa
kilometa nne kwenda kijiji cha jirani
kutafuta huduma ya maji hivyo waliiomba Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
iwachimbie kisima cha maji ili waweze kuondokana na tatizo hilo
Pia walieleza
wapo baadhi ya wazazi wamekuwa na
tabia ya kuwatelekeza watoto wao wanaokuwa
wamefaulu kujiunga na masomo ya Sekondari kwa kushindwa kwa makusudi kuwalipia ada za shule watoto wao na kuwananulia
vifaa vya shuleni
Nae mgeni rasmi wa mahafari hayo Hassanal Shabil Dala aliwataka wazazi wa
wanafunzi hao waakikishe wanafunzi
wanakao faulu kujiunga na kidato cha kwanza hapo mwakani wanawapeleka shule na ambao watakuwa hawakufaulu wawatafutie shule
Alisema wazazi
wanao wajibu wakuwalea watoto wao
vizuri iliwanapomaliza elimu ya msingi waweze
kuendelea na masomo zaidi badala ya
kuwaacha wazurule mitaani
Dala aliwaasa
wanafunzi hao wasiwe na tabia ya
kukimbilia mitaani na kucheza madisko
ambayo hayana umuhimu wowote
kwenye maisha yao wala manufaa
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Litabunga
Godfrey Lusambo alisema atajitahidi kumshauri mkurugenzi wa Halmashauri ya Nsimbo
kupeleka mradi wa maji kwenye shule hiyo
Alisema shule hizo za msingi ambazo zipo kwenye
makazi ya wakimbizi ya Katumba
zilikuwa zinamilikiwa na na shirika
la kuwaudumia wakimbizi TCRS
lakini hivi karibuni ndio
ziwemekabidhiwa kwa Halmashauri ya Nsimbo
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Elius
Nguard alimshukuru Hassanal
Dala kwa kuipatia msaada wa sola
ya umeme ambayo itawasaidia kendelea
na kuwafundisha masomo wanafunzi mida ya usiku
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment