Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Halmashauri ya Mji wa Mpanda Mkoani Katavi
inatarajia kununua nyumba 68
za Shirika la nyumba la Taifa(NHC) kwa ajiri ya kukabiliana
na tatizo linalowabili watumishi wake la ukosefu wa nyumba za kuishi
Haya yalielezwa
hapo juzi kwenye kikao cha Baraza la
Madiwani wa Halmashauri ya Mjiwa Mpanda na mwenyekiti wa kamati wa kamati ya Mipango miji
Ardhi na Maliasili na mazingira Wily
Mbogo alipokuwa akiwasilisha
kwenye Baraza la Madiwani taarifa ya
utekelezaji wa shughuli mbambali za
kamati hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu Julai
hadi Septemba mwaka huu
Alisema
katika kubaliliana na tatizo la uhaba wa
nyumba za kuishi kwa watumishi wa Halmashauri hiyo wameamua kuanza kufanya mchakato wa
kununua nyumba za 68 za Shirika la Nyumba la Taifa zilizoko katika mtaa wa
Ilembo
Mbogo aliliambia Baraza hilo la madiwani kuwa Kikao
cha Baraza la madiwani kilicho
kaa hapo Septemba 26 mwaka huu kilimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri afanye
ulinganisho wa gharama ya mkopo wa
kununulia nyumba hizo kwenye
mashirika na taasisi za kifedha
mbalimbali
Alieleza Mkurugenzi
alizingatia agizo hilo na
alifanya malinganisho kwenye
taasisi na mashirika ya kifedha mbalimbali kama alivyokuwa ameagizwa
Alifafanua
Tanzania Local Goverment Loon board liba ya mkopo wao
ni asilimia 26 Banki ya CRDB riba ya mkopo ni asilimia 18 n,Banki ya NMB riba yao ya mkopo ni asilimia 18 na TIB rIba yao ni asilimia nne
Baada ya taarifa ya mwenyekiti huyo wa kamati
ya mipango miji Ardhi
na mazingira Baraza hilo lilitowa maamuzi ya kuchukuwa Mkopo kwenye Banki
ya TIB kwa ajiri ya ununuzi wa nyumba 68 za shirika la nyumba la Taifa
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Halmashari ya Mji wa Mpanda Enock Gwambasa alilieleza
baraza hilo kuwa Halmashauri itafanya wawasiliano na Wizara ya ofisi ya Waziri Mkuu(TAMISEMI) kwa ajiri
ya kuwapatia kibali cha kuchukua mkopo huo TIB
kama ambavyo taratibu zinavyoelekeza
Alisema
Halmashauri hazina mamlaka ya kuingia mikataba ya kukopa fedha kwenye mabanki
mpaka wawe wamepewa kibali na TAMISEMI na ndio maana Halmashauri yake itafanya
hivyo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment