Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mwalimu mstaafu
wa Shule ya Msingi Vikonge Wilayani hapa
Rashiid Mbogo(62) Mkazi wa Kijiji cha Majalila Kata ya Mpanda Ndogo
Wilaya ya Mpanda amefikishwa
kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya
Mpanda kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake
mwenye umri wa maika mitano
Mtuhumiwa alifikishwa kizimbani
hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa na kusomewa mashitaka na mwendesha mashitaka
Mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi Naathaniel
Silomba
Mwendesha mashitaka
alidai mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo hapo Oktoba 19 mwaka huu majira ya saa mbili usiku huku akiwa nyumbani kwake
Mtuhumiwa anadaiwa siku hiyo ya tukio alikuwa
amekaa sabuleni akiwa akisubiria chakula
cha usiku kilichokuwa
kikiandaliwa jikoni na bibi ya mtoto huyo ambae ni mke wa mtuhumiwa
Mwendesha mashitaka aliiambia mahakama wakati akiwa anaendelea kusubilia chakula
mtuhumiwa alimwita mjuu kuu wake
sebuleni na kisha alimweka juu ya mapaja
yake na alivua nguo na kuanza kumbaka huku mtoto huyo akiwa anapiga kelele za kuomba msaada
Mwendesha mashita
Silomba aliendelea kuieleza mahakama kuwa
baada ya kusikia mayowe ya mtoto
huyo Bibi wa mtoto na majirani waliingia
ndani ya nyumba sebuleni na kukuta mtoto huyo huku akiwa anatokwa na damu nyingi kwenye sehemu zake za
siri na huku akiwa analia kutokana n maumivu makali aliyokuwa ameyapata
Baada ya kusomewa mashitaka hayo mtuhumiwa
alikana mashitaka hayo ambayo alikuwa
amesomewa na mwendesha mashitaka
Hakimu
Chiganga aliieleza mahakamani kuwa mdhamana wa mshitakiwa uko wazi kwa ajiri ya mdhamana endapo mshitakiwa
atamiza mashariti ya mdhamana
Ambapo mshitakiwa
alitakiwa awe na mdhamini mmoja mwenye mali isiyohamishika yenye thamani ya
shilingi milioni tano hata hivyo mshitakiwa alishindwa kutimiza masharti ya
mdhamana
Mtuhumiwa
alipelekwa rumande ambapo Hakimu Chiganga aliihairisha kesi hiyo hadi hapo
Novemba sita itakapo tajwa tena
Yapo makosa
ambayo ni makubwa kama vile wizi wa
kutumia silaha , unyang’anyi na kupatikana na dawa za kulevya adhabu zake ni k ndogo kuliko adhabu ya kosa la ubakaji lakini hayana dhamana huku kosa la ubakaji
lenye adhabu kubwa dhamana yake inakuwa ikowazi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment