Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma Katavi
Jeshi la Polisi
Mkoa wa Katavi linamshikilia mwalimu Mstaafu
wa Shule ya Msingi Vikonge Kata ya Mpanda Ndogo
Rashid Mbogo (62) Mkazi wa Kijiji
cha Majalila kwa tuhuma za kumbaka mjuu
kuu wake (5)na kumsababishia mtoto huyo maumivu makali yalipelekea alazwe
Katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda huku hari yake ikiwa ni mbaya
Kwa
mijibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi kamishina msaidizi mwandamizi Dhahiri Kidavashari tukio hilo lilitokea hapo juzi majira ya saa
mbili usiku nyumbani kwa mtuhumiwa
Alisema siku hiyo ya tukio mtuhumiwa alikuwa amekaa ndani na mjukuu wake huyo huku bibi ya mtoto huyo
ambae ni
mke wa mtuhumiwa akiwa jikoni anapika
chakula cha mlo wa usiku
Alifafanua kabla
ya mtuhumiwa kutenda kitendo hicho alikuwa na mazoea ya mara kwa mara ya muda mrefu ya kumwita mjuukuu wake
huyo na kumlea kwenye mapaja yake
huku akiwa anamchezea chezea na kutaniana
Alisema hari hiyo ndio ilifanya hata siku hiyo
ya tukio bibi wa mtoto huyo alipoingia ndani akitokea jikoni kwa lengo la kuchukua unga
ndani wa kusongea ugari na alipo
mkuta mume wake amemlea mjukuu wake juu ya mapaja yake hakuwa
na shaka yoyote kwani alijua ni
mazoea ya siku zote ya kumlea mjukuu wake
Alieleza
wakati mke wa mtuhumiwa akiwa
anaendelea kusonga ugari alisikia
mjuu kuu wake akipiga kele ndani lakini alizipuuzia kelele hizo kwani alidhani wanacheza na babu yake
Bibi wa mtoto huyo wakati
akiwaanaendelea kupika ugari ghafla mjukuu wake aliingia jikoni huku akiwa analia kwa nguvu na akiwa anatokwa damu nyigi kwenye sehemu zake za siri
Kidavashari alisema bibi wa mtoto huyo alipomuuliza analia nini
na kwanini anatokwa na damu
kwenye sehemu zake za siri ndipo mtoto huyo
alipomweleza bibi yake kuwa amebakwa na
babu yake
Majirani
wanaishi kwenye eneo hilo baada ya
kusikia mtoto huyo analia kwa nguvu kwa muda mrefu walifika nyumbani kw mtuhumiwa na baada ya kuambiwa mkasa wa kubakwa kwa
mtoto huyo na babu yake waliamua kutowa taarifa
kwa jeshi la polisi
Polisi walifika kwenye eneo hilo na kufanikiwa
kumkamata mtuhumiwa Rashid Mbogo
na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika
ilikujibu tuhuma inayomkabili
Kidavashari alisema
mtoto huyo bado amelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda akiwa anaendelea kupatiwa
matibabu huku hari yake ikiwa bado ni mbaya
No comments:
Post a Comment