Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mwanafunzi mmoja wa darasa la sita shule ya msingi Ugalla Wilaya
ya Mlele Mkoa wa Katavi Yohana Ramadhani(14)
anasadikiwa kuwa ameliwa na Mamba wakati akiwa akioga na wenzake katika
mto Ugalla
Kwa mujibu wa
Diwani wa Kata hiyo ya Ugalla Mohamed Asenga
tukio hilo la kusikitisha
lilitokea hapo Oktoba 17 mwaka huu majira ya saa kumi na moja jioni
katika mto huu wa Ugalla
Alisema siku hiyo marehemu akiwa na watoto wenzake kamailivyo kuwa kawaida yake alikwenda kwenye mto huu kwa lengo la
kuoga huku akiwa na rafiki zake hao ambao walikuwa wakiishi nae
Kijijini hapo
Alieleza
baada ya kuwa wamefika kwenye mto huo walivua nguo zao na kuziweka kando
ya mto na kisha waliingia ndani ya mto na kuanza kuoga kwa kuogelea ndani
ya maji
Asenga alisema wakati watoto hao wakiwa
wanaendelea kuogelea alitokea mama mmoja
alifika kwenye mto huo kwa lengo la kuteka maji kwa ajiri ya matumizi ya nyumbani kwake
Alifafanua wakati akiwa anachota maji mama huyo
alimwona Mamba akiwa kando ya mto huku akiwa anawavizia watoto hao waliokuwa wakiogelea pasipo wao
kujua kama kuna mamba aliye karibu na wao
Alisema mama
huyo alimlazimu kuwaambia watoto hao
waache kuoga na watoke haraka ndani ya
mto huu kwani amemwona mamba akiwa pembeni ya mtoto akiwavizia kuwakamata
Diwani
Asenga alieleza ndipo watoto hao walipoamua kutoka ndani ya
mto huo kwa kuhofia kulimwa na
mamba wakati wakiwa wanatoka ndipo mamba huyo aliyekuwa pembezoni mwa mto alipomkamata Yohane Ramadhan na kuingia nae ndani ya mto
Alisema wenzake walipomwona amekamatwa na
mamba walianza kupiga mayowe ya kuomba
msaada huku wakiwa wanashirikiana na mama
amekenda kuteka maji hariambayo
iliwafanya watu ambao walikuwa
karibu na eneo hilo walifika na kuanza jihihada za kutaka kumuokoa mtoto huyo lakini hawakufanikiwa kwani haweza kumwona
wala mamba mwenyewe
Diwani
Asenga alieleza kuwa mpaka sasa mtoto huyo haja patikana na uongozi wa Kijiji hicho
umeisha towa taarifa kwa Idara ya maliasiri na mazingira iliwaweze kumsaka mamba huyo na kumuuwa
ili kuepusha vifo vya wananchi wengine wa Kijiji
hicho
Mwisho
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment