ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya
Karagwe Dk.Benson Bagonza ameonyesha wasiwasi wake kuhusu hatua ambazo
serikali inachukua katika kudhibiti kuingia kwa ugonjwa wa Ebola kwenye
mipaka ya taifa letu.
Askofu huyo alisema hayo jana wakati
akizungumza na waandishi wa habari kwenye viunga vya kanisa la KKKT
usharika wa Sumbawanga ambapo kikao cha halmashauri kuu ya kanisa hilo
kinafanyika na kuwajumuisha maaskofu 23 kutoka Dayosisi zote hapa nchini
wakiongozwa na Askofu mkuu wa kanisa hilo Dk. Alex Malasusa.
Alisema
kuwa mipaka ya nchi si salama kabisa katika kudhibiti kuingia kwa
ugonjwa huo, kwani kama vitu visivyotakiwa vinaweza kupita mipakani
hivyo ni rahisi kwa vidudu vilivyo mwilini kwa mtu kuweza kuingia na
kusababisha kuenea kwa ugonjwa huo ambao ni tishio na umeua watu wengi
katika nchi za afrika magharibi.
"Sijasema kuna Ebola.....lakini
taifa letu halipo salama kama vitu visivyotakiwa vinaweza kupenya
kwenye mpaka vikaingia je kisichoonekana na kinachokuja ndani ya mwili
si ndio hatari zaidi......kama magendo, silaha haramu, wahamiaji haramu
na madawa ya kulevya yanaweza kupita je vijidudu vilivyojificha" alihoji
Dk Bagonza
Aliitaka serikali kuchukua tahadhari ya kutosha ili
kudhibiti ugonjwa huo usipenye na kuingia nchini kwani mwingiliano wa
watu kutoka nchi jirani hususani Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo (DRC)
na taifa letu ni mkubwa na katika nchi hiyo tayari watu kadhaa
wamefariki dunia kutokana na maradhi hayo.
Pia alisema kuwa
fungamano la makanisa ya afrika wamepanga kuweka sadaka maalumu Septemba
28 ili kuweza kuchangia wale walioathirika na ugonjwa huo hususani
katika nchini za afrika magharibi ikiwemo na DRC.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment