Home » » ASKOFU WA KANISA LA KKKT DAYOSISI YA KARAGWE AONESHA WASIWASI JUU YA EBOLA KATIKA MIPAKA

ASKOFU WA KANISA LA KKKT DAYOSISI YA KARAGWE AONESHA WASIWASI JUU YA EBOLA KATIKA MIPAKA

 ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe Dk.Benson Bagonza ameonyesha wasiwasi wake kuhusu hatua ambazo serikali inachukua katika kudhibiti kuingia kwa ugonjwa wa Ebola kwenye mipaka ya taifa letu.

Askofu huyo alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye viunga vya kanisa la KKKT usharika wa Sumbawanga ambapo kikao cha halmashauri kuu ya kanisa hilo kinafanyika na kuwajumuisha maaskofu 23 kutoka Dayosisi zote hapa nchini wakiongozwa na Askofu mkuu wa kanisa hilo Dk. Alex Malasusa.

 Alisema kuwa mipaka ya nchi si salama kabisa katika kudhibiti kuingia kwa ugonjwa huo, kwani kama vitu visivyotakiwa vinaweza kupita mipakani hivyo ni rahisi kwa vidudu vilivyo mwilini kwa mtu kuweza kuingia na kusababisha kuenea kwa ugonjwa huo ambao ni tishio na umeua watu wengi katika nchi za afrika magharibi.

 "Sijasema kuna Ebola.....lakini taifa letu halipo salama kama vitu visivyotakiwa vinaweza kupenya kwenye mpaka vikaingia je kisichoonekana na kinachokuja ndani ya mwili si ndio hatari zaidi......kama magendo, silaha haramu, wahamiaji haramu na madawa ya kulevya yanaweza kupita je vijidudu vilivyojificha" alihoji Dk Bagonza

 Aliitaka serikali kuchukua tahadhari ya kutosha ili kudhibiti ugonjwa huo usipenye na kuingia nchini kwani mwingiliano wa watu kutoka nchi jirani hususani Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo  (DRC) na taifa letu ni mkubwa na katika nchi hiyo tayari watu kadhaa wamefariki dunia kutokana na maradhi hayo.

Pia alisema kuwa fungamano la makanisa ya afrika wamepanga kuweka sadaka maalumu Septemba 28 ili kuweza kuchangia wale walioathirika na ugonjwa huo hususani katika nchini za afrika magharibi ikiwemo na DRC.


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa