Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MWANAKIJIJI cha Itenka Tarafa ya Nsimbo wilayani Mlele Katavi, Mary
Magese (39) ameuwawa na mwili wake kutupwa katika kisima cha maji.
Mauaji hayo yalifanyika Septemba 14 mwaka huu saa mbili usiku
kijijini hapo baada ya marehemu kumaliza kula chakula cha usiku akiwa na
mume wake Lazaro Maziku (40).
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema wanandoa hao walipomaliza kula mume alikwenda bafuni kuoga.
Aliporudi hakumkuta mkewe hivyo alianza kumtafuta bila mafanikio ndipo alipokwenda kwa majirani na ndugu zake pia hakumpata.
Alisema siku iliyofuata saa mbili asubuhi zililizagaa taarifa ya
kuwpeo kwa maiti kisimani ndipo uongozi wa kijiji ulipokwenda na kuukuta
mwili wa mke wa Maziku
Kidavashari alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha
mauaji hayo ni wivu wa mapenzi kati ya Maziku na Shija Joseph
aliyetuhumiwa kuwa hawara wa marehemu kwa muda mrefu.
Alisema jeshi la polisi linamshikilia mume wa marehemu kuhusiana na
kifo hicho kwa mahijiano zaidi na atafikishwa mahakamani baada ya
upelelezi kumekamilika
Chanzo:Tanzani Daima
No comments:
Post a Comment