Saturday, September 20, 2014
MWANAMKE AUWAWA KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI NA MUME WAKE
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtu mmoja aitwaye Benadeta Bwetel (38) Mkazi wa Kijiji cha Uruwila Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi ameuwawa kikatili kwa kwa kupingwa na kitu kizito kichwani na mume wake aitwaye Mohamed Katyukuru na kisha kufungiwa ndani ya nyumba
Kwa mujibu wa kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi kamishina msaidizi mwandamizi Dhahiri Kidavashari tukio hilolilitokea hapo Septemba 14 mwaka huu majira saa moja na nusu usiku asubuhi huko katika Kijiji cha Uruwila
Alisema kabla ya kifo hicho marehemu enzi za uhai wake walikuwa wakiishi pamoja na mume wake Mohamedi Katyukuru pamoja na watoto wao wawili Saidi Mohamedi (14) na Amuni Mohamedi (11)
Katika maisha yao ya ndoa waliokuwa wakiishi pamoja mume wa marehemu alikuwa na mazoea ya kumpiga mara kwa mara mkewe
Kidavashari alifafanua siku hiyo ya tukio Raphael Antony akiwa na Albert Mayamba ambao walikuwa ni jirani zake na marehemu walitoka kwenye miji yao na kuelekea shambani na walipita njia ya jirani na nyumba ya marehemu walishitushwa hari ya hapo ilvyokuwa ni tofauti ya kawaida ya siku zote ambapo huwa wanaaikuta familia hiyo ikiwa hapo nyumbani
Alieleza jirani hao wa marehemu walipotembea mbele kidogo kutoka kwenye nyumba ya marehemu waliona miburuzo ya baiskeli ikiwaimetokea nyumbani kwa marehemu na ndipo waliposhitushwa na hari hiyo ns kuhisi kunatatizo kwenye nyumba hiyo
Majirani hao waliamua kwenda kutowa taarifa kwenye mwenyekiti wa kijiji na mwenyekiti wa kijij aliamua kuongozana na majirani hao hadi kwa mtendaji wa Kata aitwaye Didasi Buyaga
Kamanda Kidavashari alisema kishamtendaji wa kata aliongozana nao hadi nyumbani kwa marehemu na walikuta mlango umefungwa kwa kamba kama ishara ya kuonyesha ndani ya nyumba hiyo haina mtu ndani
Alisema walipiga hodi lakini hawakuweza kujibiwa ndipo walipoamua kuvunja mlango na kuingia ndani na kukuta mareheumu akiwa amekufa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani lakini hawaku mkuta mume wake wala watoto na mpaka sasa hawajulikani waliko
Chanzo cha mauwaji hayo bado hakijajulikana kwani mume wa maehemu na watoto mpaka sasa hawajulikani wako wapi na upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment