Home » » KIJANA WA MIAKA 20 JELA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUMBAKA NA KUMSABABISHIA MAUMIVU MAKALI BINTI WA MIAKA 16

KIJANA WA MIAKA 20 JELA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUMBAKA NA KUMSABABISHIA MAUMIVU MAKALI BINTI WA MIAKA 16

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na Walter Mguluchuma,
Sumbawanga.
 
MAHAKAMA ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa  imemhukumu kwenda jela miaka 30
Martin Misala (20) mkazi wa kijiji cha Katongolo kata ya Kipili wilayani
Nkasi kwa kosa la kumbaka bint huyo  na kumsababishia maumivu
makali
 
 
Akitoa hukumu hiyo hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya Nkasi Ramadhan
Rugemalila alisema kuwa anamtia hatiani mtuhumiwa baada ya kuridhika na
ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka pasipo kuacha shaka yoyote na
kuwa anamtia hatiani kwa kosa hilo la ubakaji chini ya kifungu cha sheria
No,130(1)(2).
 
 
Upande wa mashitaka ukiongozwa na mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi
Hamimu Gwelo uliiambia mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo
la kumbaka binti huyo oktoba (20) mwaka jana majira ya saa 6 usiku katika
kijiji hicho cha Katongolo walipokua wametokea disko.
 
 
Katika kesi hiyo upande wa mashitaka uliitisha mashahidi wanne ambao
walitoa ushahidi wao huku mtuhumiwa akikosa watu wa kumtetea na ndipo
mahakama ilipoamua kumtia hatiani kwa kosa hilo baada ya kuridhishwa na
maelezo yaliyotolewa na upande wa mashitaka.
 
 
Kutokana na kosa hilo upande wa mashitaka uliiomba mahakama hiyo kutoa
adhabu kali kwa mtuhumiwa huyo ili liwe ni fundisho na kwa wengine baada ya
vitendo kama hivyo kushamiri wilayani Nkasi katika siku za hivi karibuni
 
Mtuhumiwa kwa upande wake aliiomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu kwa
sababu yeye hilo ni kosa lake la kwanza lakini pia familia yake inamtegemea
sana.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa