Home » » JELA MIAKA 15 KUIBA NG'OMBE

JELA MIAKA 15 KUIBA NG'OMBE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Wakati huohuo mahakama hiyo imemhukumu kwenda jela miaka 15 Masanja Lupinga mkazi wa kijiji cha Katani kwa kosa la uwizi wa ng’ombe
 
Upande wa mashitaka uliieleza mahakama hiyo kuwa septemba 16 mwaka jana mtuhumiwa huyo aliiba ng’ombe 8 za Lauliano Kayoka mkazi wa kijiji cha Ntemba
 
 
Alisema ngombe hao walikamatwa mjini Sumbawanga pamoja mtuhumiwa huyo wakizipeleka machinjioni kwa ajiri ya kwenda kuwauza
 
Upande wa mashitaka uliita mashahidi 8 wakiwemo na ng’ombe hao kama kielelezo mahakamani na kwa kuzingatia kuwa mtuhumiwa hili si kosa lake la kwanza mahakama hiyo ilimtia hatiani kwenda kutumikia kifungo cha miaka 15 jela chini ya kifungu No,168 na 165 ya kanuni ya adhabu sura ya 16
 

 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa