Home » » HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA KUANZA UJENZI UJENZI WA MAKAO YAO MAKUU MAPYA‏

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA KUANZA UJENZI UJENZI WA MAKAO YAO MAKUU MAPYA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  katika Mkoa wa Katavi  inatajia kuanza ujenzi  hivi karibuni      wa majengo ya ofisi za makao makuu mapya  katika eneo la Tarafa ya Kabungu
Hayo yalielezwa hivi kalibuni  kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo  Yassin Kibiriti  kwenye kikao cha baraza hilo la madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya maji  mjini hapa
Kibiriti  alilieleza baraza hilo kuwa Serikali imeisha towa  fedha kiasi cha shilingi milioni miatano       kwa Halmashauri hiyo kwa ajiri ya ujenzi wa majengo ya ofisi ya makao makuu yao mapya
Alisema  ofisi za makao makuu yao  yanatajiwa  kuhamishiwa katika Tarafa ya Kabungu  kutoka  mahari yalipo sasa Mpanda mjini
Alifafanua  Halmashari inaangalia uwezekano wa  kufanya mazungumzo  na shirika la nyumba  iliwaweze kuwekeana mkataba wa ujenzi  wa majengo  ya ofisi hizo kwa gharama nafuu
Alieleza  mchakato wa kuhamishia makao makuu yao mapya kuhamia  Kabungu  umeisha pitishwa na vikao husika kilichobaki ni swala la Halmashauri hiyo kumpata mkandarasi
Aidha alieleza kuwa umefika wakati sasa kwa  majengo ya Ofisi za vijiji na kata  yanayojengwa  mawe ya msingi yawe yanawekwa na madiwani wa maeneo husika  badala ya majengo hayo kuwekwa  mawe ya Msingi na viongozi  wa ngazi ya Mkoa ,Taifa na wakimbizaji wa Mwenge
Kibiriti alisema majengo hayo  yakiwekwa mawe ya msingi na madiwani  itasaidia sana kuwafanya madiwani wafanye kazi kwa tija kwenye Kata zao


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa