Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda katika Mkoa wa Katavi inatajia kuanza ujenzi hivi karibuni wa majengo ya ofisi za makao makuu mapya katika eneo la Tarafa ya Kabungu
Hayo yalielezwa hivi kalibuni kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Yassin Kibiriti kwenye kikao cha baraza hilo la madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya maji mjini hapa
Kibiriti alilieleza baraza hilo kuwa Serikali imeisha towa fedha kiasi cha shilingi milioni miatano kwa Halmashauri hiyo kwa ajiri ya ujenzi wa majengo ya ofisi ya makao makuu yao mapya
Alisema ofisi za makao makuu yao yanatajiwa kuhamishiwa katika Tarafa ya Kabungu kutoka mahari yalipo sasa Mpanda mjini
Alifafanua Halmashari inaangalia uwezekano wa kufanya mazungumzo na shirika la nyumba iliwaweze kuwekeana mkataba wa ujenzi wa majengo ya ofisi hizo kwa gharama nafuu
Alieleza mchakato wa kuhamishia makao makuu yao mapya kuhamia Kabungu umeisha pitishwa na vikao husika kilichobaki ni swala la Halmashauri hiyo kumpata mkandarasi
Aidha alieleza kuwa umefika wakati sasa kwa majengo ya Ofisi za vijiji na kata yanayojengwa mawe ya msingi yawe yanawekwa na madiwani wa maeneo husika badala ya majengo hayo kuwekwa mawe ya Msingi na viongozi wa ngazi ya Mkoa ,Taifa na wakimbizaji wa Mwenge
Kibiriti alisema majengo hayo yakiwekwa mawe ya msingi na madiwani itasaidia sana kuwafanya madiwani wafanye kazi kwa tija kwenye Kata zao
No comments:
Post a Comment