Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Jeshi la polisi
Mkoa wa
Katavi linawasaka watu watatu kwa
tuhuma za kumuuwa na kisha kumfukia aridhini Mbaya Lukondia (36) mkazi wa Kijiji cha Kabunde Kata ya Mamba
Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi
Kamanda wa jeshi la polisi wa Mkoa wakazi aliwataja
watuhumiwa hao wanaotafutwa kuwa ni Ubakila
Kidakira , Jimon Dogi (lala)na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la
Omary wote wakaziwa Kijiji cha
Kabunde Kata ya Mamba Wilaya ya Mlele
Kwa mujibu wa
Kamanda Kidavashari ni kwamba kabla ya kifo hicho marehemu alitoweka nyumbani kwake mwezi Aprili mwaka huu na
haikuweza kueleweka mahali alipo kuwa
Alisema kwa kipindi
chote hicho ndugu wa marehemu
waliendelea kumtafuta hadi hapo june 19 alipogundulika akiwa amefukiwa aridhini huku mwili wake ukiwa umeharibika vibaya
Alifafanua baada ya kufukuliwa kwa mwili huo wa marehemu
na kufanyiwa uchunguzi ndipo ilipoonyesha kuwa marehemu aliuwawa kwa kupingwa
na kitu kizito katika sehemu ya kichwani
na ubavuni
Alisema
watuhumiwa hao wanadai baada ya kufanya mauwaji hayo walitoweka
kijijini hapo na mpaka sasa
hawaja fahamika mahali walipo kimbilia
Alieleza wananchi wa kijiji hicho waliwatila
mashaka ya kuhusika na tukio hilo baada ya mwili wa marehemu kupatika
ukiwa umefukiwa aridhini na wao
toka siku huyo walitoweka
Kijijini
Kamanda
Kidavashari amesema jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi linaendelea
kuwatafuta watuhuiwa hao watatu
iliwakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria
mwisho

No comments:
Post a Comment